Kamata kamata ya pikipiki hapa jijini dar, ni shida
Mwanafunzi wa darasa la sita ajinyonga, habari kamili iko hapa
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Kakoleni wilayani hapa mkoani Kilimanjaro, Khalid Shaban (14),amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali akiwa chumbani kwake
Inadaiwa Shaban amejiua kutokana na mshtuko wa kifo cha mama yake mzazi aliyefariki siku chache zilizopita
Katika tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi lilitokea Novemba 28 mwaka huu, saa 7.00 mchana katika eneo la kata ya Mabogini, Moshi.
Akizungumza na gazeti hii leo (Jumanne) Diwani wa Kata hiyo, Emmanuel Mzava, amesema baada ya mama mzazi wa Mwanafunzi kuanza kuugua mtoto huyo alikata tamaa na kusema kuwa mama yake hataweza kupona tena
Mzava amesema baada ya muda mfupi mama wa kijana huyo alifariki dunia, alipofariki afya ya Shaban ilianza kudhoofika kutokana na kifo cha mama yake
"... Alipoteza matumaini na kwamba hawezi kuendelea tena kuishi bila ya mama yake,"amesema Mzava.
MWIZI: Pikipiki hii inapatikana Vetenary magorofani zinapogeuzia daladala za kutoka Mwenge jijini Dar es Salaam
Pikipiki hii inapatikana Vetenary magorofani zinapogeuzia daladala za kutoka Mwenge jijini Dar es Salaam. Pikipiki hii inahistoria ya kushangaza mno, pikipiki hii iliibiwa mkoani Tanga na mwizi akaileta Dar es Salaam.
Kisha akaiweka kwenye kijiwe icho hapo ilipo ili naye akatoe huduma kwa abilia kama walivyo watu wengine kijiweni hapo.
Ile anashuka tu kwenye pikipiki iyo baada ya kufika kijiweni hapo yule jamaa alidondoka chini na kupoteza maisha pale pale na baada ya jamaa huyo kupoteza maisha watu walijaribu kuiweka pembeni pikipiki iyo lakini chakushangaza haisogei hata nukta moja.
Tangu kutokea kwa kifo cha huyo mwizi wa pikipiki hii kutoka Tanga yapata miezi mitatu hadi leo na kila wakijaribu kuitoa pikipiki hii kijiweni hapo haisogei kabisaa.
Kumetokea tetemeko la Ardhi na limepiga maeneo ya mkoa wa Kagera na inadaiwa mikoa jirani nayo imepata mtikisiko huo
Tetemeko kubwa la Ardhi laikumba mikoa ya Mwanza na Kagera. Kumetokea tetemeko la Ardhi na limepiga maeneo ya mkoa wa Kagera na inadaiwa mikoa jirani nayo imepata mtikisiko huo.
Linadaiwa kurudia tena likiwa na mtikisiko mkubwa zaidi uku Nyumba kadhaa zikiwa zimebomoka kutokana na ukubwa wa tetemeko hilo pia Taarifa za vifo zimesikika.
Tetemeko hilo limeanza kusikika mida ya saa tisa na nusu, huku likidaiwa kuwa na ukubwa/uzito wa 5.7 na lilikuwa likitokea upande wa kaskazin magharibi.
Mpaka sasa imeripotiwa kuwa takribani watu 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa, kaa nadi tukujuze zaidi kupitia hapa hapa Miko Yetu.
Picha ya siku inaletwa kwenu kwa hisani ya Mikoa Yetu, Tazama Line pamoja na Mutalemwa Blog
Siku zote mtangulize mungu wako ndipo utafanikiwa.
Ivi unafikiri huyu dreva wa gari hili baada ya kutokea kwa ajali hii alikuwa katika hali ya namna gani?? Tupe maoni yako.
Wananchi wa Gabon wachoma moto jengo la bunge, habari kamili bofya hapa
GABON: Baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa kuwa mshindi kwa 49.85%, wananchi walichoma jengo la Bunge.
Nini hatma ya demokrasia katika nchi za Afrika? Ebu tupe maoni yako Tahadhari.
Kama ukuisikia habari hii basi ipo hapa kwa ajili yako mpendwa, bofya hapa
Kuna ajali iltokea maeneo ya Sanzale Bagamoyo siku ya juma nne tarehe 30 mwezi wa 9 mwaka huu.
Ajali iyo iliyohusisha Lori pamoja na gari la kampuni ya Pepsi ambapo Dereva wa gari la kampuni ya pepsi alijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali japo chanzo cha ajali iyo akikuweza kujulikana kwa araka ila inasadikiwa kuwa ni uzembe wa madreva.
R.I.P POLISI WETU WA 4 WALIOPOTEZA MAISHA YAO UKO MBANDE
Usiku huu nimefika Mbande - Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo. Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.
Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu. Ameyasema ayo MWIGULU NCHEMBA.
WATANZANIA 9 WAMETEKWA KISHA KUUAWA NA WATU WANAODAIWA KUWA NI ASKARI WA RWANDA
KYERWA, KAGERA: Watanzania 9 wametekwa kisha kuuawa wakiwa wanavua katika mto Kagera na watu wanaodhaniwa ni askari kutoka Rwanda.
Picha kutoka maktaba
Waziri Mwigulu asema atalifuatilia suala hilo na kulitolea maamuzi. Source: Jamii Forum.
Ofisi za NSSF Ilala na Posta zavamiwa, kujua zaidi bofya hapa
Kundi kubwa la watu limevamia ofisi za NSSF zilizopo Ilala na Posta leo asubuhi na kuzua vurugu kubwa kwa kile walichodai kuwa ni kutokana na ucheleweshwaji wa mafao yao baada ya kuacha kazi.
Watu hao waliojitambulisha kama waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Optima Aviation, wamesema wamechukua hatua hiyo baada ya kudai kero hiyo ni ya muda mrefu wakizungushwa kuhusiana na mafao yao.
Wamedai wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuona dalili za kuwepo mchezo mchafu baina ya shirika hilo la NSSF na Mwajiri wao ambaye ni Kampuni ya Optima kufuatia kupewa barua ya kuacha kazi kwa ajili ya kupata mafao yao lakini kila wanapokwenda NSSF wanaelekezwa kurudi kwa mwajiri wao.
Taarifa kutoka NSSF zinasema kuwa baada ya kufuatilia wamegundua kampuni hiyo ya ulinzi haijapeleka/haijawasilisha makato ya wafanyakazi wake zaidi ya sh. 100 milioni.
Hivi sheria inasemaje kama kama Ofisi haipeleki makato ya wafanyakazi, nakumbuka kuna mkuu aliwahi kulizungumzia hili.
Askari aliyemuua Mwangosi aukumiwa kifungo cha miaka 15, zaidi bofya hapa
Hukumu kwa Askari aliyekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Mwandishi Mwangosi ni leo tarehe 27/7/2016.
Hukumu hiyo ambayo hasa itahusu adhabu anayostahili Askari husika itasomwa na Jaji Kihwelo wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa.
========= Updates ========
MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa leo imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27) aliyemuua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi wa kituo cha Chanel Ten.
Mwandishi Mwagosi aliuawa mwaka 2012 huko Iringa katika purukushani za Polisi na wafuasi wa CHADEMA.
Watu 13 wafariki dunia nchini Somalia, bofya hapa kujua zaidi
SOMALIA: Milipuko 2 imetokea karibu na kambi ya vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Afrika(AU). Takribani watu 13 wamefariki dunia.
Al-Shabaab imetangaza kuhusika na mlipuko hiyo. Je unafikili sababu ya kulipua milipuko kama hii kwenye eneo kama hili kuna maanisha nini?? Tupe maoni ysko hapo chini.
Mtoto wa miaka 5 anusulika kubakwa na kijana wa miaka 18, habari kamili iko hapa
Taarifa mnamo tarehe 13.07.2016 majira ya saa 10:00 jioni katika mtaa wa Kitangiri kata ya Kitangiri wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, mtuhumiwa Elisha Lameck miaka [18] mkazi wa kitangiri alikutwa akijaribu kumbaka mtoto mdogo (Jina lake linahifadhiwa) mwenye umri miaka 5, nyumbani kwao.
Inadaiwa kuwa siku hiyo mtuhumiwa alifika hapo kwenye hiyo nyumba kuwasalimia na kumkuta msichana wa kazi za ndani aitwaye Zulekha Sameer na mtoto, ndipo alipomchukua mtoto huyo na kuingia naye chumbani kisha akafunga mlango.
Baada ya dakika kadhaa dada wa kazi Zulekha Sameer alishangaa ukimyaa uliokuwepo katika chumba walichoingia ndipo alipokwenda kufungua mlango nakukuta ukiwa umefungwa, ndipo alikwenda dirishani kuchungulia na kumuona mtuhumiwa Elisha Lameck akiwa amevua nguo zote pamoja na mtoto huku akizichezea sehemu za siri za mtoto.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa mfanyakazi (House Boy) wa mama mwenye nyumba aliyejulikana kwa jina la Mama Shakifu ambaye anaishi Uarabuni kwa sasa, na kwasababu aliwahi kufanya kazi katika nyumba hiyo, mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kwenda katika nyumba hiyo kuwasalima.
Mtuhumiwa amekamatwa na yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, huku uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ukiwa bado unaendelea.
Breaking news: watu 9 wahofiwa kufa maji kwenye mto Ruvuma
Watu 9 wahofiwa kufa maji baada ya boti waliokuwa wakitumia kuvuka katika Mto Ruvuma kuzama.
Endelea kufuatilia habari zetu kujua kitakachojiri. Kwenye tukio hili.
Kama ukuipata hii basi isome hapa, miaka 60 jela kisa kumuingilia mkewe kinyume na maumbile
Mkazi wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Jaribu Obed mwenye miaka 26 amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na kosa la kumuingilia mkewe kinyume na maumbile.
Hakimu Mkazi wa mahakama ya wilaya hiyo Erick Marley amesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo bila kuacha shaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo
Alisema ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwake na wanaume wengine wanaokusudia kutenda kosa kama hilo
Mwendesha mashtaka wa polisi Peter Makala alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kati ya Mei 28 na 30 usiku katika kijiji cha Kumuhama
Alidai mshtakiwa huyo alifanyia kitendo hicho mkewe huyo kwa siku tatu mfululizo wakati akiwa na mimba ya miezi saba
Alidai kitendo hicho kilimuathiri kiafya na kukosa uvumilivu hivyo kutoroka na kwenda kutoa taarifa kwa dada yake anayeishi mtaa wa Migombani mjini Kibondo
Mwendesha mashtaka huyo alidai baada ya dada yake kupata taarifa hizo alimpeleka katika ofisi za ustawi wa jamii kisha polisi na ambako alipewa fomu namba tatu PF3 ili kwenda kutibiwa hospitali
Wanavyuo mkoani Dodoma wakumbwa na maswahibu tena, habari kamili iko hapa
JESHI la Polisi mkoani Dodoma limewasambaratisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya mkoani humo ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wamekusanyika katika mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) yaliyopangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya African Dream mjini humo ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye.
Polisi wakiwa wamezingira ukumbi huo.
Kwa mjibu wa maelezo ya Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, wanafunzi hao walifanya mkusanyiko usiokuwa halali kwa kuwa hawakuwa na kibali cha kuwarushusu kukusanyika eneo hilo ndiyo maana polisi wakaamua kuwasambaratisha ili kuzuia mikusanyiko ya kisiasa isiyokuwa halali.
Watu 30 na Lita 18,000 za pombe haramu ya gongo zakamatwa Rombo
Zaidi ya lita 18,000 za pombe haramu ya gongo zimekamatwa wakiwemo watu 30 kwa kujihusisha na upikaji wa pombe hiyo katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kati mwezi Aprili na Juni nane mwaka huu na watu hao watafikishwa mahakamani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Bw Evarest Silayo amesema hayo katika uzinduzi wa albamu ya ngome zimepasuka ya kwaya nyota ya alfajiri ya kanisa la TAG wilayani humo ambayo pamoja na kueneza neno la injili lakini pia kwaya hiyo itakuwa inakemea maovu ndani ya jamii ukiwemo upikaji na unywaji wa pombe hiyo.
Bw Silayo amesema, lita hizo na watu hao wamekamatwa kwa ushirikiano wa polisi,jeshi la mgambo na raia wema wa wilaya hiyo katika oparesheni ya kudumu inayofanywa na serikali ili kuhakikisha upikaji na unywaji wa pombe hiyo unakomeshwa.
Kiongozi wa kanisa hilo Mchungaji Frigili Kimario amesema,kwaya hiyo pia itajihusisha na kukemea mila potofu katika jamii ukiwemo ukeketaji kwa wasichana ambao madhara yake ni makubwa na baadhi ya wanawake wamepoteza maisha katika wilaya hiyo.
Waumini wanawake wa kanisa hilo pamoja na kuipongeza serikali katika kupambana na pombe hiyo lakini wameiomba iongeze juhudi kwa kuwa madhara ya pombe haramu ya gongo ni makubwa ikiwemo kupoteza nguvu kazi ya taifa,ndoa kuvunjika na vijana kukataa kuoa.
Jamani vitu vingine akina mama mnajitakia kabisaa, ebu soma hii
Jamani vitu vingine akina mama pamoja na akina dada mnajitakia nyinyi wenyewe, kwamfano unakuta mdada kavaa kinguo kifupi alafu anajipanga kwenda safari ya mbali.
Ivi jiulize kwakuvaa vinguo vifupi na vyenye kuonyesha maumbile yenu mnakuwa mkijenga picha gani kwa akina kaka zenu pamoja na wadogo zenu wanaokuwa wanawatazama???
Mfano mzuri mtazame mama huyu, kavaa kanga yake moja tu alafu kama unavyomuona akipiga misele yake kwenye watu wengi wenye kila aina ya tabia. Kwaiyo ikitokea mkabakwa asitokee mtu wakulalamika maana mnakuwa mmeyataka wenyewe.
Mimi sidhani kama mtu anaweza kuwa amevaa vizuri nguo ambazo zinastara arafu mwanaume akambaka kilahisi kama tunavyojionea kwenye matukio ya kila siku.
WALINZI WAWILI WAUAWA KWA KUKATWA MAPANGA MKOANI MARA, ZAIDI BOFYA HAPA
Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamewauwa kwa kukatwa katwa mapanga walinzi wawili wa kimasai ambao walikuwa wakilinda maduka katika eneo la Kiyara kata ya Kwangwa katika manispaa ya Musoma Mkoani Mara na kufanikiwa kupora vitu mbalimbali katika maduka hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,kamishina msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP.Ramadhan Ng’azi,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia machi tisa mwaka huu na kusema kuwa Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja wa tukio hilo akiwa na baadhi ya vitu vilivyoibwa na kwamba upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kiyara Bw.Cosmas Majura na diwani wa kata hiyo Bw.Christopher Muyaga,wamesema vitendo vya ujambazi katika eneo hilo vinazidi kuongezeka kila kukicha kutokana na wananchi wake kutokukubali kushiriki katika mpango wa ulinzi shirikishi.
WATU 2 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 13 WAKIJERUHIWA VIBAYA, ZAIDI BOFYA HAPA
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ndenjela linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es Salaam kuligonga kwa nyuma basi dogo aina ya toyota Hiace ambalo ni daladala linalofanya safari zake kati ya Igawilo na stendi kuu jijini Mbeya katika eneo la Uyole, kwenye barabara kuu ya Tanzania - Zambia.
Ajali hiyo imetokea majira ya alfajiri wakati basi la kampuni ya Ndejela likitokea gereji kwenda katika kituo kikuu cha mabasi jijini Mbeya kwa ajili ya kuchukua abiria ili kuanza safari ya kwenda Dar es Salaam, lakini lilipofika eneo la Kilimo katika bonde la Uyole, ndipo basi dogo aina ya toyota Hiace ambalo lilikuwa limesimama kituoni,likaingia ghafla barabarani na ndipo lilipogongwa na kwa nyuma na basi hilo la Ndenjela ambalo lilikuwa kwenye mwendo mkali na kusababisha daladala hilo kuacha njia na kugonga jiwe kubwa kando ya barabara.
Afisa muuguzi msaidizi wa zamu katika hospitali ya rufaa Mbeya,Abdul Kumwambe amethibitisha kuwepo kwa vifo vya watu wawili pamoja na majeruhi 13 ambao wanatokana na ajali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi,Ahamed Msangi amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi wa basi la kampuni ya Ndenjela huku akidai kuwa uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea.


























