Watu 30 na Lita 18,000 za pombe haramu ya gongo zakamatwa Rombo

Zaidi ya lita 18,000 za pombe haramu ya gongo zimekamatwa wakiwemo watu 30 kwa kujihusisha na upikaji wa pombe hiyo katika wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kati mwezi Aprili  na Juni nane mwaka huu na watu hao watafikishwa mahakamani.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Bw Evarest Silayo amesema hayo katika uzinduzi wa albamu ya ngome zimepasuka ya kwaya nyota ya alfajiri ya kanisa la TAG wilayani humo ambayo pamoja na kueneza neno la injili lakini pia kwaya hiyo itakuwa inakemea maovu ndani ya jamii ukiwemo upikaji na unywaji wa pombe hiyo.

Bw Silayo amesema, lita hizo na watu hao wamekamatwa kwa ushirikiano wa polisi,jeshi la mgambo na raia wema wa wilaya hiyo katika oparesheni ya kudumu inayofanywa na serikali ili kuhakikisha upikaji na unywaji wa pombe hiyo unakomeshwa.

Kiongozi wa kanisa hilo Mchungaji Frigili Kimario amesema,kwaya hiyo pia itajihusisha na kukemea mila potofu katika jamii ukiwemo ukeketaji kwa wasichana ambao madhara yake ni makubwa na baadhi ya wanawake wamepoteza maisha katika wilaya hiyo.

Waumini wanawake wa kanisa hilo pamoja na kuipongeza serikali katika kupambana na pombe hiyo lakini wameiomba iongeze juhudi kwa kuwa madhara ya pombe haramu ya gongo ni makubwa ikiwemo kupoteza nguvu kazi ya taifa,ndoa kuvunjika na vijana kukataa kuoa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top