Kumetokea tetemeko la Ardhi na limepiga maeneo ya mkoa wa Kagera na inadaiwa mikoa jirani nayo imepata mtikisiko huo

Tetemeko kubwa la Ardhi laikumba mikoa ya Mwanza na Kagera. Kumetokea tetemeko la Ardhi na limepiga maeneo ya mkoa wa Kagera na inadaiwa mikoa jirani nayo imepata mtikisiko huo.

Linadaiwa kurudia tena likiwa na mtikisiko mkubwa zaidi uku Nyumba kadhaa zikiwa zimebomoka kutokana na ukubwa wa tetemeko hilo pia Taarifa za vifo zimesikika.

Tetemeko hilo limeanza kusikika mida ya saa tisa na nusu, huku likidaiwa kuwa na ukubwa/uzito wa 5.7 na lilikuwa likitokea upande wa kaskazin magharibi.

Mpaka sasa imeripotiwa kuwa takribani watu 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa, kaa nadi tukujuze zaidi kupitia hapa hapa Miko Yetu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top