KUTOKA PWANI: HIKI NDICHO KIJIJI CHA KAZOLE PAMOJA NA VITONGOJI VYAKE

Utangulizi: Kijiji cha Kazole ni miongoni mwa vijiji vinavyo patikana katika kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Kijiji hiki cha kazole kipo umbali wa kilometa 2 kutoka kwenye barabara ya rami ya Vikindu, pia kijiji hiki kimezungukwa na vijiji vinginevyo kama kijiji cha Vikindu, Vianzi, Lugwadu na Magodani.

Nikijiji kilichopo kwenye eneo zuri na lenye sifa nyingi mno, na kati ya sifa za eneo la kijiji hiki ni kama zifuatazo.

(a) Maji- kijiji chetu cha Kazole hakina tabu kabisa ya maji, lakini pia eneo kubwa la kijiji hiki maji yake yanapatikana kwa urahisi sana hata kama ni kwa kuchimba kutumia machine au kwa kutumia mkono.

Hapa ni Vikindu getini kwa mbelw kidogo ndipo kuna barabara inayoelekea Vianzi na Kazole,  kama nilivyoelekeza kwenye picha ya chini.

(b) Ukaribu wa kijiji na mkoa wa Dar es Salaam- kijiji hiki cha Kazole kipo karibu sana na mkoa wa Dar es Salaam, ambapo kwa sasa mkoa wa Dar es Salaam unaishia pale Kongowe njia panda ya kwenda Kigamboni na umbali wa kutoka hapo Kongowe hadi Vikindu ni kama kilometa 3 na nusu hivi na kutoka Vikindu hadi kijijini Kazole ni kilometa 2.

Japo kuna taarifa za kwamba mkoa wa Dar es Salaam unatarajiwa kupanuliwa hadi Vikindu mwisho na kuchukua eneo lote linaloizunguka Vikindu vikiwemo vijiji tajwa hapo juu pamoja na kijiji cha Kazole  na vitongoji vyake vyote kuunganishwa kwenye wilaya mpya ya Kigamboni.

Hii ndio njia inayoelekea Vianzi na iyo inayoingia kushoto ndio inaelekea Kazole. 

(c) Maeneo ya uwekezaji- kijiji hiki cha Kazole kina maeneo mengi makubwa na mazuri ya uwekezaji wa kila aina, mfano uwekezaji wa viwanda, elimu, huduma za jamii kama hospitali, viwanja vya michezo, huduma ya Mawasiliano kama minara ya simu ambayo itasaidia kupatikana kwa huduma ya Mawasiliano kwa wakazi wa kijiji cha Kazole pamoja na vijiji vya jirani kama vilivyo tajwa hapo.

CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WAKAZI WA KIJIJI CHA KAZOLE NA VITONGOJI VYAKE NI IZI HAPA

Ukisha ingia iyo njia ya kushoto kama maelekezo yanavyoelekeza hapo juu, mbele utaona njia mbili kama zinavyoonekana hapa, wewe fuata njia inayoelekea mkono wa kulia.

Mbali ya faida zilizo tajwa hapo juu bado kijiji hiki cha Kazole kina kabiliwa na changamoto nyingi sana na kati ya changamoto hizo ni pamoja na izi zifuatazo hapo chini.

1. Upimaji wa maeneo ya wanakijiji pamoja na kutambua mipaka ya kila kijiji, mpaka sasa vijiji tajwa ambavyo ni Kazole, Vikindu, Vianzi, Lugwadu pamoja na Magodani havina ramani rasmi yenye kuonyesha mipaka sahihi ya vijiji vyao ambayo itawasaidia kuepukana na kero za migogoro ya ardhi.

Ukisha fuata njia ya kulia mbele kabisa utakutana na njia mbili ziko kama unavyoziona hapo kwenye picha.

Kwa ufupi vijiji hivi vinatakiwa kutenga maeneo ya wazi, barabara, hospital, shule, masoko, maeneo ya ibada, viwanja vya michezo, maeneo ya maziko nk. Ni vyema viongozi wahakikishe yanatenga maeneo haya kabla idadi ya watu haijawa bukwa zaidi ili kujiepusha na migogoro ya ardhi inayoweza kujitokeza hapo baadae.

2. Usafiri- wakazi wa vitongoji vilivyomo ndani ya kijiji cha Kazole mfano kama kitongoji cha Cheta na kilongoni pamojana wakazi wa kijiji cha Magodani wanakabiliwa sana na tatizo la usafiri wa kudumu nyakati za asubuhi, mchana pamoja na usiku, hakuna usafiri wa kuaminika, usafiri wa kuaminika upo kuanzia Vikindu getini kuelekea Mbagala au Mkuranga nk. Ila kuanzia kijiji cha Kazole, Cheta, Magodani huku ni bodaboda pamoja na magari ya mizigo.

Hili ndio daraja la Mkokozi, na hapa ndipo mwisho wa kijiji cha Vikindu na pia ndio mwanzo wa Kijiji cha Kazole na viunga vyake.

3. Ubovu wa miundombinu ya barabara, ndugu msomaji uwezi amini kuwa kuna barabara moja tu ambayo ndiyo inaunganisha vijiji vitatu, barabara iyo uanzia Vikindu getini na upita kijiji cha Kazole kisha kitongoji cha Cheta na huendelea hadi kijiji cha Magodani.

Barabara hii ni yakawaida tu yaani barabara ya vumbi nasio ya rami, lakini pia haina matengenezo ya kulidhisha kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma ya usafiri na usafirishaji wa bidhaa zao.

Muonekano wa daraja la Mkokozi, na hapa ndipo mwisho wa kijiji cha Vikindu na pia ndio mwanzo wa Kijiji cha Kazole na vitongoji vyake.

Kipindi cha masika mvua zikifuruliza kunyesha waga wakazi wa kitongoji cha Cheta na vijiji vyote vinavyounganishwa na barabara hii waga usafiri unakuwa ni mgumu sana maana maji ufurika barabarani kutokana na kukosa mwongozo wa wapi yaelekezwe.

Madaraja yaliyopo kwenye barabara hii sio imara na hayapo kwenye kiwango cha kuweza kuhimili kishindo cha maji mengi.

Daraja hili la Mkokozi, limejengwa pembezoni mwa mkondo wa maji, pia ni dogo mno.

4. Hospital au Zahanati- ndugu msomaji wa makala hii huwezi amini kwamba vijiji tajwa hapo juu hakuna hospital au zahanati, kwaiyo wakazi wa vijiji hivi wanalazimika kufuata huduma hii pale Vikindu ambapo ni umbali mrefu sana.

5. Shule za msingi na Secondary- kwa upande wa elimu bado hali sio nzuri maana kuna shule za msingi mbili tu wakati vijiji ni vitatu na kuna umbali mkubwa kutoka kijiji kimoja hadi kingine.

Izo nguzo za umeme unazoziona hapo chini zipo hapa kwenye makutano ya hii barabara. 

Shule ya kwanza ya msingi ipo kijiji cha Kazole ina darasa la kwanza hadi darasa la tatu na shule msingi ya pili ipo kijiji cha Magodani shule hii ina hadi darasa la saba, ila kitongoji cha Cheta hakina shule hata moja na pia nikitongoji ambacho kipo katikati ya vijiji tajwa hapo juu.

Na kwa upande wa shule za sekondari vijiji vyote tajwa hapo juu pamoja na vitongoji vyake vitanategemea sekondari moja tu ambayo inaitwa shule ya sekondari Honda iliyopo kata ya Vianzi.

Nguzo zenyewe za umeme ni hizi hapa. Ukifuata njia ya kulia kwenye picha iliyopo hapo juu utakutana na daraja lililopo hapo chini.

6. Umeme- tangu mwaka jana mpaka sasa ni nguzo pekee za umeme ndizo zimesambazwa hadi eneo la shule ya msingi iliyopo kijiji cha Kazole, uku umeme ukitakiwa kufika hadi kijiji cha Magodani ukipitia kitongoji cha Cheta.

Na taarifa zinadai kuwa kufikia mwezi wa sita mwaka huu 2016 utandazaji wa nguzo za umeme ulitakiwa uwe umeisha fika ndani ya kijiji cha Magodani ukipitia kitongoji cha Cheta, kisha ndipo zoezi la kuvuta umeme lianze, lakini hakuna kitu.

Hapa ni Mkokozi wa pili kwenye kitongoji cha Ngunguti, angalia daraja lilipojengwa kisga angalia magari yanapopita, na hapo ni kabla ya mvua za masika kuanza kunyesha.

7. Mawasiliano- mbali ya kwamba vijiji hivi vipo jirani kabisa na mkoa wa Dar es Salaam hasa kitongoji cha Cheta lakini bado wakazi wake wanakabiliwa na changamoto ya Mawasiliano hasa kwa upande wa simu za mkononi.

Mawasiliano mazuri ya kupiga na kupokea simu pamoja na matumizi ya Internet mwisho ni eneo la Vikindu pekee,  ukisha anza safari ya kuelekea Kazole, Cheta na Magodani basi Mawasiliano hupungua hadi kiwango cha chini kabisa kiasi kwamba simu inakuwa iko On lakini mtu akikupigia hawezi kukupata hewani.

Angalia ukubwa wa eneo la kupitisha maji kwenye daraja hili la mto Mkokozi wa pili. 

CHANZO CHA KUZOROTA KWA MAENDELEO KWENYE KIJIJI CHETU CHA KAZOLE NA VITONGOJI VYAKE

1. Mfumo mbovu wa uongozi uliopo madarakani- Vijiji hivi vinashindwa kukua kwa kasi kubwa kimaendeleo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo izi hapa;
(a) ubinafsi
(b) ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya uchambuzi wa mambo ambayo yatachochea ukuaji wa maendeleo
(c) uwajibikaji na uroho wa madaraka.

Baada ya kupita ilo daraja kwa mbele kabisa utakutana na njia izi, wewe fuata njia ya kushoto kisha endela kwenda nayo. 

2. Viongozi kutosikilizana wao kwa wao pamoja na kupuuza maoni ya wananchi wao- kumekuwa na wadau mbalimbali wakijitokeza kuja kuwekeza katika maeneo ya vijiji hivi, lakini viongozi wa vijiji hivi wamekuwa wakiwakatisha tamaa na matokeo yake wawekezaji hao wanaondoka na kuelekea sehemu yenye mfumo mzuri wa uongozi kwa wananchi wao.

Mfano: katika kitongoji cha Cheta walijitokeza wawekezaji wawili walitaka kujenga hospital pamoja na kituo cha mafuta, lakini uongozi wa ngazi ya kijiji uliwazuia watu hao kwa madai ya kwamba kitongoji hakina mamlaka ya kuamua jambo hilo.

Kwa mbele kabisa utakutana na nyumba hii iko mkono wa kulia imeandikwa "Hapa mageti matatu kwa Palijala famili"

3. Mfumo wa uongozi: vijiji hivi inaendesha mambo yao kwa kutumia mfumo wa uzawa nasio mfumo rasmi wa kisheria (mfumo wa kujuana).

Viongozi wote kuanzia ngazi ya vijiji mpaka vitongoji vyote hupatikana kwa njia ya kujuana. Mfano mzuri ni kijiji cha Kazole mjini, mwenyekiti wa kitongoji hicho ndugu Mtandika amejiuzuru ghafra bila taarifa yoyote ya msingi, hii ni kwa sababu aliwekwa pale kwa manufaa ya mtu mmoja nasio kuitumikia jamii nzima.

Mbele kidogo ya nyumba iyo hapo juu kuna njia iko hivi, wewe kunja kushoto kisha endelea na safari.

Je sheria ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu mfumo wa uongozi wa namna hii???. Na je wajibu wa kiongozi katika nafasi yake ni hupi??

Baada ya kuendelea na safari mbele utafika eneo linaloitwa magenge 20 kama inavyo onekana kwenye picha hii, kisha kunja kuelekea kulia ukiufuata mkorosho huo.

4. Rushwa: vijiji tajwa vyote vinauza viwanja kwa watu wageni kwenye maeneo ya vijiji vyao lakini pesa zinazokusanywa kutokana na ushuru wa mauzo hayo azijulikani zinapo kwenda, wananchi wanapojaribu kuhoji kwenye mikutano ya vijiji juu ya mapato na matumizi hawapewi majibu sahihi zaidi tu yakudanganywa kwa kuambiwa leo hatujaanda taarifa rasmi kwaiyo msubiri siku nyingine, tabia hii imetajwa sana.

Muonekano wa eneo la magenge 20 huu hapa

Tabia hii imekuwa endelevu, kila wakidai haki zao juu ya maendeleo ya vijiji vyao ujibuwa hivyo hivyo. Je kisheria ni sahihi kujibiwa vile???.

Hapa ni mwisho wa kitongoji cha Kazole na ndipo mwanzo wa kitongoji cha Cheta.

Ukisha fuata iyo njia niliyo elekeza hapo juu kwenye picha ya tatu ukianza na hii, kwa mbele kidogo utakutana na njia hizi, hii njia ya kulia ni njia inayoelekea kwenye eneo la Bakhresa anapomwaga matakataka yake, na njia iliyopo kushoto ndio njia inayoelekea kitongoji cha Cheta pamoja na kijiji cha Magodani. 

Je kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na viongozi wasio wajibika ipasavyo na matokeo yake wanajinenepesha wao na familia zao kwa kutumia pesa zinazotokana na mapato ya ardhi ya vijiji vyao pamoja na miradi mingine ya vijiji??

Hayo ni baadhi tu ya maswali wanaojiuliza wananchi wa kijiji cha Kazole pamoja na vitongoji vyake na vijiji vya jirani kama vilivyo tajwa hapo juu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top