MINI SHOP CHETA
Kifaa kikubwa cha chuma kimeanguka kutoka angani katika eneo la migodi Kaskazini mwa Myanmar
Kifaa hicho cha muundo wa mviringo, kilichopatikana siku ya Ijumaa katika jimbo la Kachin, kina urefu wa mita 4.5 na upana wa mita 1.2.
kifaa kingine cha chuma chenye maandishi ya kichina kilitoboa paa la nyumba iliyo karibu wakati mmoja lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Inakisiwa kuwa kisa hicho huenda kinahusiana na satellite ya China iliyorushwa angani.

Wakaazi walisema kuwa walisikia sauti kubwa kabla ya kifaa hicho kuanguka
Maafisa kutoka kwa idara moja ya ulinzi iliyo karibu, wanasema kuwa kifaa hicho kilipingirika umbali wa mita 50 kabla ya kutua eneo moja lenye matope .
"Tulishikwa na hofu kwa sababu ya mlipuko huo," mwanakijiji Ko Maung aliliambia gazeti la Myanmar Times.
Vifa hivyo vinaaminiwa kuwa vya satellite au sehemu za injini ya nge au kombora.
Binti aliyetoroka vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia, Ilhan Omar ashinda Useneta
Mwanamke akaa kwenye jeneza siku nzima akitafuta uzoefu wa kifo
Imetokea Brazil na Mwanamke mwenyewe anaitwa Vera Lucia da Silva na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza.
Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote.
Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.
Matukio: Mtoto azaliwa mara mbili, habari kamili bofya hapa kufahamu zaidi
Mbali na habari nyingine motomoto jionee tukio la mtoto nchini Marekani 'kuzaliwa' mara mbili.
Alitolewa tumboni mwa mama yake akiwa na wiki 16 ili kufanyiwa matibabu, na kisha akarejeshwa tumboni, na hatimaye kuzaliwa rasmi baada ya miezi kutimia.
Upungufu wa wahudumu waifanya Kenya Airways kuahirisha safari 5 za ndani na nje ya nchi
Shirika la ndege la Kenya Airways limeahirisha safari zake tano za kwenda ndani na nje ya nchi leo October 16 2016 kutokana na upungufu wa Wahudumu wa ndege kazini.
Taarifa inasema sababu hasa ya kuahirisha safari hizo tano za Mombasa, Kilimanjaro, Juba, Maputo, Harare na Lusaka ni kutofika kazini kwa Wahudumu wa ndege ambao wamepangiwa.
WANAWAKE WAVUA NGUO BARABARANI WAKITAFUTA WAUME WA KUWAOA, HABARI KAMILI IKO HAPA
Wanawake wa nchini Urusi wavua nguo barabarani kwa nia ya kutafuta waume wakuwaoa.
Ungependa mwanamke utayemuoa awe na sifa gani? Ebu twambie japo kwa ufupi tu.
Rais Dilma Rousseff aondolewa madarakani kwa kura 61, zaidi bofya hapa
BRASILIA, BRAZIL: Rais Dilma Rousseff ameondolewa madarakani kwa kura 61 leo baada ya Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Aliyekuwa Makamu wake, ambaye aligeuka adui namba moja Michel Temer, sasa anaapishwa kuwa Rais hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika mwaka 2018.
Vikosi 4,000 vya kulinda usalama kupelekwa Sudan kusini
Baraza la Usalama.la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kupelekwa vikosi 4,000 vya kulinda usalama nchi Sudani Kusini.
Nchi za Kenya, Rwanda na Ethiopia kuchangia wanajeshi katika vikosi hivyo.
Watu 13 wafariki dunia nchini Somalia, bofya hapa kujua zaidi
SOMALIA: Milipuko 2 imetokea karibu na kambi ya vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Afrika(AU). Takribani watu 13 wamefariki dunia.
Al-Shabaab imetangaza kuhusika na mlipuko hiyo. Je unafikili sababu ya kulipua milipuko kama hii kwenye eneo kama hili kuna maanisha nini?? Tupe maoni ysko hapo chini.
Hofu yazidi kutanda baada ya watu 80 kupoteza maisha, zaidi bofya hapa
Wizara ya afya ya Afghanistan imesema takriban watu themanini wameuawa na zaidi ya wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye mji mkuu Kabul. Baadhi ya taarifa zinasema kulikuwa na milipuko miwili.
Shambulio hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa ukatili.
Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.
Kenya: msichana wa miaka 13 afariki dunia, chanzo iki hapa
Bofya hapo juu kwenye iyo picha.
KISUMU, KENYA: Msichana mwenye miaka 13, amefariki baada ya kutumia kining'iniza nguo(Hanger) akijaribu kutoa mimba yake iliyokuwa na wiki 4.
Alivuja damu nyingi na alifariki njiani wakati akiwa anakimbizwa hospitali.
Bofya hapo chini kwenye iyo picha.
Korea yafanya majaribio ya makombora yake mawili, zaidi bofya hapa
Korea kaskazini imefanya majaribio ya makombora yake mawili mbali na umoja wa mataifa kupiga marufuku matumizi yoyote ya makombora,taarifa zinasema kombora la kwanza halikufanikiwa huku la pili likisafiri umbali wa kilomita mia nne.
Msemaji wa Waziri wa Umoja wa taifa wa Korea Kusini Joeng Joon-hee amesema majaribio hayo ni kukiuka vikwazo.
Kila mtu anakuwa na bahati yake tena peke yake, ebu na wewe jaribu bahati yako kwa kubofya kwenye maelezo yaliyopo hapo chini
Mwanasisa wa DRC yamkuta maswahibu mazito kweli kweli, habari kamili bofya hapa
Hatimae Mahakama ya ICC yamhukumu miaka 18 jela mwanasiasa wa DRC, Jean Pierre Bemba kwa uhalifu wa kivita & uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Waendesha mashitaka wanamlaumu makamu huyo wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa kufumbia macho vitendo viovu vilivyofanywa na vikosi vyake katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika Kati kuanzia Oktoba 2002 hadi Mei 2003.
Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi, iliyohusisha mashitaka matano ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu, baada ya kuwapeleka wanajeshi 1,500 kutoka katika jeshi lake binafsi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika jitihada za kuzima mapinduzi dhidi ya mtawala wa wakati huo.
Jamani vitu vingine akina mama mnajitakia kabisaa, ebu soma hii
Jamani vitu vingine akina mama pamoja na akina dada mnajitakia nyinyi wenyewe, kwamfano unakuta mdada kavaa kinguo kifupi alafu anajipanga kwenda safari ya mbali.
Ivi jiulize kwakuvaa vinguo vifupi na vyenye kuonyesha maumbile yenu mnakuwa mkijenga picha gani kwa akina kaka zenu pamoja na wadogo zenu wanaokuwa wanawatazama???
Mfano mzuri mtazame mama huyu, kavaa kanga yake moja tu alafu kama unavyomuona akipiga misele yake kwenye watu wengi wenye kila aina ya tabia. Kwaiyo ikitokea mkabakwa asitokee mtu wakulalamika maana mnakuwa mmeyataka wenyewe.
Mimi sidhani kama mtu anaweza kuwa amevaa vizuri nguo ambazo zinastara arafu mwanaume akambaka kilahisi kama tunavyojionea kwenye matukio ya kila siku.
Nchi ya Kenya yasherekea siku ya Madaraka Yake, zaidi bofya hapa
Leo tarehe 1 june 2016 nchi ya Kenya inasherehekea siku ya Madaraka (MADARAKA DAY) ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 53 ambapo Kenya kwa mara ya kwanza ilipata nafasi ya kujiongoza yenyewe kabla ya kupata uhuru wake kamili 12 Decemba 1963, Ambapo Jomo Kenyatta akawa Waziri mkuu wa kwanza wa taifa hilo.
Rais Uhuru kenyata anawaongoza wakenya wote kuadhimisha siku hii muhimu kwao huko Nakuru Kenya,huku wapinzani wakiadhimisha siku hiyo katika viwanja vya uhuru Nairobi.
UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KATI YA TANZANIA NA UGANDA WAANZA, ZAIDI BOFYA HAPA
Tanzania na Uganda zimeanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka katika nchi ya Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola za Kimarekani bilioni nne.
Makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo yalifikiwa na marais wa nchi hizo Dr,John Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda walipokutana jijini Arusha wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mawaziri wa sekta zinazohusiana na nishati,makatibu wakuu na watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi za Tanzania na Uganda wamekutana jijini Arusha na kusaini makubaliano ya kuanza kwa mchakato ambao waziri wa nishati wa Uganda Bi.Irine Liuloni amesema mradi huo utaongeza chachu ya uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki .
Aidha viongozi hao wamesema kitakachofuata baada ya hatua hiyo ni taratibu za ndani za serikali za Tanzania na Uganda na kwamba mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya kimataifa ya uchimbaji wa mafuta ya total unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2017.
Kama mradi huo utakamilika na kuanza uzalishaji unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na ajira kwa wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
MAMA AU DADA, HOUSE GIRL YAWEZA KUWA MKE MWENZIO, ZAIDI BOFYA HAPA
Ivi ni vibaya House girl kuolewa na baba mwenye nyumba?
Ndugu msomaji wa Mikoa Yetu, karibu kwenye makala hii maalumu, nimeamua kuandika habari hii ili kujaribu kupunguza mifarakano kwenye familia zetu especially familia zenye wafanyakazi wa ndani wanaojulikana kama house girl.
Katika mada hii Mikoa Yetu, imekuwa ikikutana na maswali mengi sana ambayo mda mwingine yalikuwa yakituchanganya hata sisi wenyewe katika kuwajibu wahusika, maswali haya malanyingi yalikuwa yakiulizwa na akina mama.
Na kwa upande wa akina baba maswali yao sio mengi ukilinganisha na akina mama, sasa napenda nianze kwa kusema mambo yafuatayo ili wote twende sawa.
WAJIBU WA MWANAUME KATIKA FAMILIA: Mwanaume anawajibu wa kutimiza mahitaji yote ya msingi katika familia yake, moja ya majukumu hayo ni pamoja na kutoa pesa za matunzo ya familia yake kadri ipasavyo, kuonyesha upendo wa dhati kwa mama pamoja na watoto wake, na mambo mengineyo nk.
WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA FAMILIA: Mwanamke ndiye mtendaji mkuu wa familia kwa upande wa nyumbani ukiachilia mbali ya kwamba baba ndiye kichwa cha familia, mwanamke anamajukumu mengi kwa upande wa nyumbani moja ya majukumu yake ni pamoja na kupika chakula cha familia, kufua nguo za mumewe pamoja na nguo za watoto, kuakikisha nyumba pamoja na eneo linaloizunguka nyumba ni safi, kuonyesha upendo wa dhati kwa mumewe pamoja na watoto wake, nk.
Picha kutoka maktaba
Ndugu msomaji wa makala hii, nadhani mpaka hapo tayari umeisha anza kupata mwanga kuhusu jibu la swali la makala yetu, sasa twende kuona wajibu wa mfanya kazi wa ndani kama house girl.
House girl wajibu wake ni kuakikisha anafanya usafi wa kuizunguka eneo la nyumba kwa nje na kufanya usafi huo kwa upande wa ndani kwa baadhi tu ya maeneo ya nyumba hiyo pamoja na kuwaogesha watoto, kufua nguo za watoto, na kufanya kazi ndogo ndogo za nyumbani.
House girl hatakiwi kufanya usafi chumbani kwa mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kufua au kupiga pasi nguo za mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kumuandalia chakula au chai mume wa mama mwenye nyumba, nk.
Sasa ukiona house girl anafanya kazo zote nilizosema kuwa hatakiwi kuzifanya pindi awapo nyumbani kwako, ukiwa kama mama mwenye akili timamu jua kabisa tayari umeamua kumuletea mumeo mke mdogo na pia usipige kelele wala kulaumu maana jitihada zote za kumuandaa mke mwenzio umezifanya wewe mwenyewe.
Ushauri wangu kwenu akina mama na akina dada nikwamba, hatukatai kuwa wafanyakazi wa ndani hawafai, ila jitaidi mfanyakazi wako awe na mipaka ya kazi, mwanaume anaamua kumuoa house girl kwa sababu yeye amechukua majukumu yote ya mama mwenye nyumba, sasa wewe mama usianze kumtupia maneno mtoto wa watu pamoja na mumeo maana yote hayo umeyataka wewe mwenyewe.
Kama umependa makala hii tafadhali Share na wenzio wajifunze kitu. Endelea kutembelea tovuti zetu zifuatazo kwa kubofya kwenye jina la tovuti husika.
SERIKALI INADAIWA 28 BILLIONS NA HOSPITAL MBALIMBALI ZA NJE YA NCHI
Serikali inadaiwa shilingi bilioni 28 na Hospitali mbalimbali za nje ya nchi kutokana na watu waliokwenda kupata huduma ya matibabu yakiwemo ya moyo huku watoto zaidi ya 500 wakihitaji huduma ya upasuaji.
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,watoto na wazee Mh.Ummy Mwalimu ametoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea msaada wa zaidi ya sh.Milioni mia mbili kwa ajili ya kusaidia watoto 101 kupata huduma ya upasuaji wa moyo na kuongeza kuwa kutibu mgonjwa mmoja nje ni milioni 16 lakini kwa hapa nchini ni sh Milioni 4 tu.

Hafla hiyo ya kupokea msaada imefanyika taasisi ya moyo iliyopo hospitali ya taifa Muhimbili daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Prof Mohamed Janabi, amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni uhaba wa damu kwani wakati mwingine huwezi kufanya upasuaji kama huna akiba ya damu pamoja na sasilimali fedha kutokana na idadi kubwa ya wanaofika kupata huduma hawana uwezo kifedha.
Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wameshapatiwa huduma ya upasuaji na wanaosubiri huduma hiyo wameiomba serikali kuzisogeza mikoani kwani wanatoka mbali tena kwa gharama kubwa kufuata huduma hiyo.





























