MWIZI: Pikipiki hii inapatikana Vetenary magorofani zinapogeuzia daladala za kutoka Mwenge jijini Dar es Salaam

Pikipiki hii inapatikana Vetenary magorofani zinapogeuzia daladala za kutoka Mwenge jijini Dar es Salaam. Pikipiki hii inahistoria ya kushangaza mno, pikipiki hii iliibiwa mkoani Tanga na mwizi akaileta Dar es Salaam.

Kisha akaiweka kwenye kijiwe icho hapo ilipo ili naye akatoe huduma kwa abilia kama walivyo watu wengine kijiweni hapo.

Ile anashuka tu kwenye pikipiki iyo baada ya kufika kijiweni hapo yule jamaa alidondoka chini na kupoteza maisha pale pale na baada ya jamaa huyo kupoteza maisha watu walijaribu kuiweka pembeni pikipiki iyo lakini chakushangaza haisogei hata nukta moja.

Tangu kutokea kwa kifo cha huyo mwizi wa pikipiki hii kutoka Tanga yapata miezi mitatu hadi leo na kila wakijaribu kuitoa pikipiki hii kijiweni hapo haisogei kabisaa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top