Kama wewe ni mpenzi na mshabiki wa msanii Diamond Platinum, ebuingia hapa uone kufuru

Pete na cheni mpya za Diamond Platnumz alizozivaa kwa wakati mmoja zina thamani ya shilingi milioni 158!

Hitmaker huyo wa Marry You amepost Instagram picha mbili zikionesha madini hayo kwa kile anachosema kuwainspire mashabiki wake.

“Thanks God for my new GOLD & DIAMONDS collection…i never thought i would be able to hang 50,000$ on my neck,” ameandika kwenye picha ya kwanza.

Kwenye picha nyingine ameandika, “Thanks God for your daily blessings never thought i would be able to walk with 22,000 $ on my Hand!!!… jus get inspired @sallam_sk don’t hate.”

Muimbaji huyo wikiendi iliyopita alitumbuiza show ya nguvu humo Muscat, Oman.

Malalamiko mengi kuhusu Alikiba kupokonywa ushindi huko MTV EMA, habari nzima iko hapa

Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu Alikiba kupokonywa ushindi huko MTV EMA.Naomba hapa nitumie nafasi hii kufafanua kilichotokea ili kuweza kuondoa huu utata. 

Kwa mujibu wa Mtv Ema Alikiba ameshinda kwa kura nyingi sana alizopigiwa na mashabiki na wamemtangaza kuwa katika kipengele cha kura nyingi Ali ndio mshindi. 

Naomba tufahamu kwamba Tuzo kubwa kama MTV EMA na BET kuna vipengele ambavyo maamuzi yake hayategemei kura za mashabiki bali huamuliwa na wadhamini, majaji pamoja na waandaaji wa Tuzo.

Kipengele hiki huangaliwa ni kiasi gani msanii anafanya vizuri katika category aliyowekwa cz inawezekana msanii akakosa kura nyingi lakini anastaili kupata tuzo kutokana na mchango wake katika mziki. 

Kipengele hicho ndicho kilichomfanya Wizzy ashinde Tuzo hiyo ya MTV EMA.

Kiukweli MTV EMA hawajakosea katika hilo cz watanzania wengi walimpigia kura Kiba bila kujali team zao lakini kwa viwango vya kimataifa kiba hawezi kumfikia hata Robo Wizkid. 

Alikiba alitakiwa kuwaambia ukweli mashabiki zake na sio kulalamika kwenye media kuwa haelewi kilichotokea wakati anafahamu ukweli wote. Kulalamika kwa Ali kutamsababishia picha mbaya na sidhani kama MTV EMA watakuja tena kumchagua kuwania Tuzo hizo katika Category yoyote ile. 

Natumaini nimeeleweka japo kwa uchache. 

wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba zaidi bofya hapa

Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed a.k.a Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba. 

Mwigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa filamu ambao wanafanya vizuri kwa sasa, amedai kama wasanii wakiamua kufanya kazi kwa bidii basi kila kitu kinawezekana. 

“Pengo la marehemu Kanumba litazibika tu ingawa najua tobo la panya huwezi kuziba na mkate ila tutajitahidi kuziba,” Gabo alimjibu shabiki katika Kikaango cha EATV. 

Aliongea,”Niwashauri watu wawe makini kwenye nidhamu, wawe makini kwenye elimu na pia wasikate tamaa katika mambo wanayofanya”  Mwigizaji huyo amemtaja Single Mtambalike kuwa ndiye mwigizaji wake bora kwa sasa.

Mfahamu Mwanamziki wa Bongo Flavour mwenye mafanikio makubwa zaidi kiliko wenzake, Bofya hapa

Anaitwa AMBWENE YESSAYA AKA AY ni mmoja wa wasanii ambaye ana mafanikio makubwa sana kimuziki kuliko msanii yeyote yule hapa nchini Tanzania,vile vile yeye ndiye msanii wa kwanza Tanzania kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa mpaka ulaya.Historia yake ya muziki ilianzia miaka 1998 

Pesa yake ya kwanza kurekodi ngoma studio alipewa na mama yake Tshs 20000/=. Ni mkulima (ana mashamba ya mpunga zaidi ya heka 100 huko ifakara Morogoro.

Ni mjasiriamali mwenye biashara nyingi ikiwemo duka la nguo. Ni mmiliki wa vipindi vya TV vya MKASI na NGAZI KWA NGAZI vinavyorushwa EAST AFRICA TV 

Anamiliki kampuni ya UNITY ENTERTAINMENT inayojihusisha na uwakala wa kazi za sanaa,matangazo na kuunganisha wasanii, pia kuleta wasanii wa nje, huu sio mwisho wa mafanikio yake bali tumegusia tu kiasi flani hivi.

Shilling 1,000 ndiyo iliyosababisha Kifo cha marehemu Thomas Mashali

Rafiki wa karibu wa marehemu Thomas Mashali aliyejitambulisha kwa jina la Ally amesimulia mkasa mzima wa kifo cha rafiki yake huyo.

Ally alisimulia mkasa wa rafiki yake huyo akiwa msibani maeneo ya Tandale jijini Dar es salaam, ambapo amedai kuwa juzi usiku alipata taarifa za kushambuliwa kwa Mashali na watu wasifahamika maeneo ya Kimara jijini humo.

“Ilikuwa usiku nimekaa nyumbani Manzese Madizini akaja dereva bodaboda anaitwa Yusuf Kidevu akaniambia babaako wanampiga huko Kimara wanamuua kama vipi nenda.”

“Nikahisi ni uongo kwasababu wakati mwingine wanazusha tu, mara kidogo akaja mtu wa pili akasema babaako anakufa huko Kimara, kwasababu alikuwa ni mtu wa pili kuniambia nikaona bora niende.”

“Nikaenda hadi Kimara, kufika pale nikakuta wameshampiga wamemuumiza askari wanampakia kwenye gari. Nikalifata gari hadi Sinza, akapata kitanda akalazwa nikaenda kumsalimia lakini sauti ilikuwa inatoka kwa mbali hadi usogeze sikio ndio unaweza kumsikia.”


“Nikamuuliza imekuwaje, akasema kuna dereva bodaboda alimkodi lakini walivyofika Kimara akampa hela kidogo wakaanza kuzozana ndio mkasa ulipoanzia.”

“Alimpa shilingi 2000 lakini dereva bodaboda alikuwa anataka shilingi 3000, akaanza kumtukana Mashali akaona anadharauliwa akampiga ngumi yule dereba bodaboda akaanguka chini, baada ya hapo akaanza kupiga kelele za mwizi wakaja watu wengine watatu wakataka kumpiga akapambana nao akawapiga.”

“Baada ya kuona wote hawamuwezi wote wakaanza kupiga kelele za kumuita mwizi, wakaongezeka watu wengine wakaanza kumshambulia.”

Mwili wa Thomas Mashali unatarajiwa kuzikwa Jumatano jijini Dar es salaam.

Ujumbe wa siku kwa hisani ya Mikoayetu.blogspot.com

Duniani kuna maneno mengi sana ila mwadamu hutakiwi kujua kila neno lina maana gani, maana ukianza kufatilia maana ya kila neno utajikuta ufanyi mambo ya maendelea mwishoe unakufa ukiwa maskini.

Vijana kwa wazee, ebu tuache maneni kisha tufanye kazi jamani. Endelea kuwa nasi.


Jifunze njia rahisi ya kufunga Tai, bofya hapa ili kujua hatua za kufuata

Jifunze njia rahisi ya kufunga Tai, SHARE na marafiki zako nao wajifunze kupitia kwako.

Endelea kuwa nasi kila siku ili tuzidi kukuhabarisha kila habari inayotufikia.

Tatizo la nguvu za kiume linakuzwa kinyume na hali halisi jinsi lilivyo

Inavyoonekana siku hizi japo kweli kuna tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haswa kwa mazingira ya mijini, Lakini hili tatizo linaonekana kukuzwa kuliko lilivyo hadi imepelekea woga mkubwa kwa baadhi ya wengi wetu.

Ndipo kwenye tafakari yangu nikaona NIANZISHE HUU UZI kwa machache tu kwa ufahamu mchache nilio nao, Ili NIWAALIKE wengi WENU kwa msaada zaidi wa mawazo kwa ndugu zetu wanaokutana na mfadhaiko huu. Nikiamini pia wengi wenu mna utaalamu na mnaoweza kuchambua haya makitu kwa ufanisi zaidi mkatatusaidia sana kwenye uzi huu.

Yafaa sasa tujikite kwenye ufumbuzi kuliko kuripoti tatizo na kulaumu. Kadiri tunavyoendekeza kuripoti tatizo tunawaathiri hata wale waliokuwa wazima ambao kwa kuwa hakuna kipimo sawia kujua kipi ni kipi, nao wasiwasi unawafanya wanapoteza ujasiri wao na kujiona wana tatizo kumbe wapo imara sana kuliko mkuki.

Kwa kuanzia yafuatayo yaweza kusaidia kuboresha kulifurahia tendo la ndoa zaidi na kwa muda zaidi.

Kuuweka Mwili vizuri: Ni wazi kuwa tendo hili linachagiwa sana na mzunguko mzuri wa damu. Mwili ukiwa kwenye hali nzuri kiafya na tendo huwa linaenda ipasavyo. Na mwili ukiwa dhoofu basi tegemea tukio dhoofu pia.

Hivyo ukitaka kuwa na matokeo mazuri kwenye ndoa yako, jitahidi sana kujiweka vizuri kwa kula sahihi na kufanya mazoezi mepesi mepesi tu kwa wale wanaoweza kuutumia muda vizuri wapiti pite Gym walau siku mbili na kuendelea kwa wiki.

Kufahamu kuwa kupumzika kwa uume baada ya baada kufika mara ya kwanza sio tatizo. Kwa wanaume walio wengi, baada ya mshindo wa kwanza hupumzika kidogo kabla ya kuendelea na awamu nyingine.

Japo kuna ambao wana uwezo wa kuendelea moja kwa moja bila kupumzika (law ya use and misuse inahusika kwa wengine apa). Kwa hio kusinyaa kwa uume baada ya mshindo wa kwanza, isifahamike kuwa ni upungufu wa nguvu bali ni ajdustiment ya mwili wenyewe kutokana na kwamba mwanaume kabla ya tendo mapigo ya moyo huongezeka na huchangia damu kwenda kwa kasi.

Na kwa hali hio anakua yupo juu sana kimhemko, inapofikia anamaliza raundi ya kwanza mwili unakua unapoa /umesharudi kwenye hali yake ya kawaida, ndiko kunakosababisha hio maneno kusinyaa kwa wengi wakati mapigo ya moyo yanaporudi kawaida (MWILI KUPOA).

Maandalizi ya mwili. Wanaume tupo tayari muda wote ila linapokua swala ya mwenza wako (kwa kuwa muda unaotumia kwa maandalizi na tendo una uhusiano wa moja kwa moja na satisfaction ya mwenzio) unahitaji muda angalao nusu saa na kuzidi kujiandaa na mwenzi wako.

Kama timu ya mpira inapoenda ugenini huhitaji muda kuzoea mazingira, ndio na mwanaume anavyohitaji muda kuzoea mazingira ya ugenini.

Hili linakusaidia sana mwanaume kutoka kwenye mihemko na kurudi kwenye hali yako ya kawaida ambayo itakusaidia kuwa na muda mzuri zaidi wa kufurahia tendo. Jitahidi pia kuvuta pumzi nyingi ndani na uiachie polepole kukusaidia kukuweka kwenye utulivu mzuri.

Timing ya kuanza tendo: Kwa kuwa tendo linahusisha sana hisia za mwili, ukiwa umetumia muda unaotosha kuandaana, basi usiwe na papara mwanzoni, bali uwe na utulivu, pia jitahidi kuzungumza moja mawili wakati unaanza kuzoea mazingira mengine (core business) EPUKA UHARAKA na kuweka sana akili yako hapo, jinafikie mwenyewe kuwa its just a normal thing (mental pride)

Concetration/ Umakini uliopitiliza… Unapaswa kumfanya mkeo aweke akili yake yote hapo, na wewe unatakiwa katika kumuweka mkeo kwenye concentration uuharibu umakini wako (level of concentration).

Ukiweka concentration ya juu sana kwenye tendo; haikuchukui dakika mbili umemaliza, na kuirudisha tena ile hali ya concentration uliokua nayo mwanzo itakuwia ngumu sana. Usiweke sana akili yako hapo kama unataka kufurahia kwa muda zaidi. ila kama hutaki kudumu.. weka akili na umahini wako hapo woote.. just seconds or a minute you are done

MAZOEZI ya mwili ni muhimu sana sana sana sana sana kwetu wanaume. Kama huna muda wa kwenda jimu walau ukiamka piga PUSH-UPS walau 50'' kila siku na 'SQUARTS'' . haya ni mazoezi mepesi lakini ni BORA zaidi kwa mwanaume.

Kwetu sisi wanaume tunatumia sana misuli yetu wakati huu, kwa hio kuna ulazima wa kutafuta ustahimilivu wa misuli ''mussle strength n perseverance''. Hio kitu ni starehe na unatakiwa baada ya tendo uwe umekuwa refreshed na sio uwe unaumwa kila mahali na sijui joints zinauma sijui nini nini? ukijiona unakuwa hivyo baada ya tendo ujue mwili wako haujakaa fiti ipasavyo kimazoezi/kiafya

Pia Afya ya Akili inahusika sana, Japo inahitaji jitihada makhususi... lakini kila mtu ana uwezo wa kuchagua nini cha kufikiria na nini si cha fikiria(kupuuzia) na pia akienda hatua zaidi anaweza kupuuza kila kitu kwa wakati fulani kama unajua una huo uwezo na ukaamua kuutumia.

Pia kuchagua kufikiri yale yaliopo kwenye uwezo na urefu wa kamba yako pekee; vitu usivyo na uwezo navyo utajisumbua tu bure na kujipa stress zaidi. Weka nguvu na jitihada zako kwenye kutafuta ufumbuzi wa changamoto zako, jifunze na acha kufikiria matatizo kwa maana hakubadilishi kitu na yataendelea kuwa hivyo n.k

Ukiwa na namna nzuri ya kuyachanganua mambo yako utasaidika sana kwenye afya ya akili yako na kuwa vizuri zaidi.

Msanii Ney wa Mitego aomba radhi juu ya wimbo wake wa Pale kati patamu

“Wakati naandika wimbo “Pale Kati” nilikua nimeangalia nyimbo zilizowahi kutoka nyuma na zilizoko sokoni sasa, sikuona kama mistari yake ina matatizo.

Lakini baada ya kukaa pamoja na kusikiliza mstari kwa mstari tumegundua kwamba kuna baadhi ya mistari ilikua ina maneno makali. Hivyo basi naomba radhi kwa mtu yeyote aliyeumizwa na mistari hiyo." - Nay wa Mitego. Nini maoni yako?

Alichokizungumza msanii Ney wa Mitego baada ya wimbo wake kufungiwa

"Ni kweli nimezipata taarifa za kufungiwa kwa wimbo wangu lakini nafikiri haya ni mambo ya kisheria kwa sasa hivi mimi sina cha kuongea maana kwa upande wangu sidhani kama kuna sababu za msingi za kufungiwa kwa wimbo wangu"- Nay Mitego.

Unadhani kuna siku Nay anaweza kubadilisha aina ya muziki wake?

TUNAPENDA HARUSI KULIKO NDOA, EBU JIFUNZE KITU LEO

Jifunze zaidi kwa kupitia ujumbe uliopo hapo juu

Wanawake wanapenda harusi na wanachukia ndoa na wanaume wanapenda ndoa na wanachukia harusi, harusi ni sherehe ya siku moja na ndoa ni mkataba ambalo lengo lake ni hudumu milele.

Wengi walipenda harusi ila walipoingia kwenye ndoa hawakuwa na furaha sababu walipenda zaidi kuvaa gauni/suti za harusi kuliko kuwa tayari kuyavaa majukumu ya ndoa na uwajibikaji.

Ndoa nyingi za mbwembwe huwa na mwisho mchungu na hasa pale wahusika walioingia kwenye ndoa kwa hitaji moja la kuoa/kuolewa sababu ya msukumo wa wazazi au pesa za muda mfupi au kushika  mimba na  kuwa kiunganishi cha ndoa.

Wanawake/Wanaume wanapenda kuzaa ila wanachukia malezi na ndio maana unakuta msichana mwenye mtoto  ana miaka 23 ila mtoto wake analelewa na mama yake na yeye anakula ujana sababu hawezi kulea mtoto wake mwenyewe.

Wanaume wengi wanajua kuzalisha ila kutunza hawawezi na akifanikiwa kutunza jua hawezi kulea mtoto.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kulea mtoto na kutunza mtoto ,kutunza mtoto ni kazi rahisi sana  sababu unamtumia mtoto pesa ya chakula ,mavazi pamoja na karo ya shule.

                   Picha kutoka maktaba

Ila kumpa mtoto malezi ni ile hali ya kutengeneza chemistry nzuri na mtoto kwa uwepo wako na kumuandaa kisaikolojia kujua umuhimu wa baba kwa kuona na kusikia.

Ndoa nyingi zilizofungwa kwa harusi ndio zinazo ongoza kwa kuvunjika na moja ya sababu ya kuvunjika kwa ndoa hizo ni watu kupenda zaidi harusi kuliko kuithamini ndoa.

Mtu anafikilia  zaidi honey moon badala ya kutafakari jinsi ya kuboresha ndoa na kuwa na kizazi chenye maisha bora na matamu.

Kuoa au kuolewa na mtu anayekupenda kwa dhati ya moyo wake ni baraka kubwa mno ambayo anakuwa ameiandaa Mungu wetu muumba mbingu na nchi.

Kama umeoa au umeolewa basi mpende na pia muheshimu sana mwenzi wako maana ujui kitakacho kutokea mda mfupi ujao kutoka sasa, usije ukafa ukiwa na dhambi ya kumdharau mumeo/mkeo.

Jifunze zaidi kwa kupitia ujumbe uliopo hapo chini. 

Mashabiki wavunja geti la kuingilia uwanjani, zaidi bofya hapa

Bado zoezila kugawa simu linaendelea, ili kushinda simu fuata maelekezo yaliyopo hapo juu

MASHABIKI wamevunja geti la kuingia
uwanjani na wameanza kupambana na polisi ambao wamelipua mabomu ya machozi na kuwamwagia maji ya kuwasha.

Co-ordinator wa mchezo huo ametoa tahadhari kama hali itaendelea hivi basi atasimamisha mchezo huo kazi nzito, ama kweli vya bure vinaua kabisa.

Bado zoezila kugawa simu linaendelea, ili kushinda simu fuata maelekezo yaliyopo hapo chini. 

ALIYECHEZA MOVIE YA YESU (JESUS), NDIYE HUYU, HISTORIA YAKE HII HAPA

Bado zoezi la kugawa simu linaendelea, ili kushinda simu fuata maelekezo yaliyopo hapo juu.

Anajulikana kama Brian Beacon, yeye ni muigizaji maarufu duniani aliyeigiza filamu ya Yesu (Jesus). Alizaliwa mnamo tarehe 13/02/1946 kwenye mji wa Oxford nchini Uingereza (UK). Alijifunza sanaa katika chuo cha Oxford Youth Theatre cha humo nchini mwao.

Msanii huyu amepata kuigiza filamu kama The Triple Echo ilikuwa mwaka 1972, na miaka miwili baadae akafanya filamu inayofahamika kama Vampyres ambapo ilikuwa mwaka 1974, Lakini pia mwaka 1979 alifanya filamu ambayo ilikuwa gumzo dunia nzima filamu ya Yesu (Jesus) hadi ikafikia watu wengi tukawa tunahisi ndiye yesu kweli kutokana na jinsi alivyovaa uhusika (character).

Na mnamo mwaka 1985 alicheza filamu ya A Zed and Two Noughts. wasambazie na wenzio ili wamjue vizuri huyu msanii kwa kipaji chake alichokitumia kwa kuvaa mfano wa maandiko matakatifu na kuufikishia ulimwengu ujumbe stahiki.

Bado zoezi la kugawa simu linaendelea, ili kushinda simu fuata maelekezo yaliyopo hapo chini.

Wasanii chipkizi ni jukumu letu kuwapa surpot ya kutosha mpaka watoke

Kwajina la kiusanii anafahamika kama Neyba, japo ingelikuwa vyema kama tungeweza kulifahamu jina lake halisi.
Mimi binafsi nimeanza kumfahamu kwa kupitia wimbo wake mpya wa Uje, ambao picha zake ndizo hizi unazozitazama hapa.
Kiukweli nimependa wimbo wake huu kuanzia kwenye mpangilio wa merodi, ujumbe uliomo ndani yake, mavazi pamoja na uchezaji wa wote walioshiliki.
Mbali ya kutowajua majina yao hawa akina dada walicheza kwenye video ya wimbo huu, kwanza niwapongeze sana kwa kuonyesha nidhamu ya kazi yao.
Lakini pili niseme neno moja kwao, ya kwamba mbali ya wao kucheza vizuri nimevutiwa na kumpenda mdada moja wao.
Mdada mwenyewe ambaye nimevutiwa nae pia nafsi yangu imempenda ni huyu hapo kwenye picha ya chini.
Sababu kubwa ya mimi kumpenda ni kama ifuatavyo 1. Uzuri wake kimuonekano, 2. Uchezaji wake ni wakuchangamka, 3. Ananidhamu kazini, na mwisho kwa sasa ni mtu anayeweza kucheza kila aina ya style bila wasiwasi.
Lakini mbali ya kuvutiwa na kumpenda mdada huyu aliyecheza kwenye wimbo huu napenda kuwapongeza wasanii chipkizi wa kila aina ya mziki wa hapa nchini kwa kazi nzuri wanazozifanya.
Na kwa upande wangu kama mmoja wa watu wanaomiliki blog hapa nchini Tanzania naomba niseme kwamba kwa msanii yeyote yule ambaye atakuwa anaitaji msaada kutoka kwangu, basi mimi niko tayari kumsaidia.
Msaada wenyewe sio lazima pesa ata kupromote nyimbo zake, kupeana ushauri, kupublish kitu chochote anachotaka kuifahamisha jamii.
Kwa maoni/maswali/ushauri napatikana kupitia simu namba hii: 0659 91 9292
Karibu sana na pia endelea kuwa nasi tukujuze zaidi kupitia hapa hapa kwenye tovuti yetu ya Mikoa Yeu. 

Jamani vitu vingine akina mama mnajitakia kabisaa, ebu soma hii

Jamani vitu vingine akina mama pamoja na akina dada mnajitakia nyinyi wenyewe, kwamfano unakuta mdada kavaa kinguo kifupi alafu anajipanga kwenda safari ya mbali.

Ivi jiulize kwakuvaa vinguo vifupi na vyenye kuonyesha maumbile yenu mnakuwa mkijenga picha gani kwa akina kaka zenu pamoja na wadogo zenu wanaokuwa wanawatazama???

Mfano mzuri mtazame mama huyu, kavaa kanga yake moja tu alafu kama unavyomuona akipiga misele yake kwenye watu wengi wenye kila aina ya tabia. Kwaiyo ikitokea mkabakwa asitokee mtu wakulalamika maana mnakuwa mmeyataka wenyewe.

Mimi sidhani kama mtu anaweza kuwa amevaa vizuri nguo ambazo zinastara arafu mwanaume akambaka kilahisi kama tunavyojionea kwenye matukio ya kila siku.

Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top