MINI SHOP CHETA

Mini Shop Cheta au Duka Dogo
Mini Shop Cheta logo
Mini Shop logo
Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.
Mini Shop Cheta
Mini Shop Cheta
Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.

Mini Shop Cheta Management
Mini Shop Cheta Management
Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. bidhaa izo zipo chini ya picha hii.
Mini Shop Cheta Map
Mini Shop Cheta Map
Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara
Chumvi
Mchele
Sukali
Mini Shop Cheta Manager
Mini Shop Cheta Manager

Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari
Vichongeo
Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Mini Shop Cheta Management finishing
Mini Shop Cheta Management finishing
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka
Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria
Maharage ya Njano
Mini Shop Cheta before plaster
Mini Shop Cheta before plaster

Maharage ya Kombati
Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.
Mini Shop Cheta map Foundation
Mini Shop Cheta map Foundation
Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop Cheta tukuhudumie leo.

Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu

Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani na Kilongoni hadi Vikindu
inayopitia Cheta, Kazole kisha kuunganisha kwenye barabara kuu ya rami inayoenda mikoa ya kusini.

Aliyasema haya kwenye mkutano wake uliofanyikia tarehe 03/11/2017 eneo la Magodani kisha kuumalizia Kazole,  ambapo alisema tayari barabara hii ya kutoka Vikindu hadi Magodani kupitia Kazole na Cheta tayari imeisha wekwa kwenye bajeti na itatengenezwa mda sio mrefu.
Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu
Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu
Mbali na hili swala la barabara pia aliongerea kuhusu watu walio uziwa viwanja kwenye eneo la Hamidu kisha baadae wakaja kuvunjiwa nyumba na kunyang'anywa viwanja vyao.

Ambapo alisema atalishugulikia swala hilo baada ya kuwapata walioshiriki kuwauzia raia viwanja hivyo kutoka kwenye eneo la muwekezaji Hamidu.

Kuhusu swala la barabara hii ya Magodani kupitia Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu nitarudi baada ya miezi mitatu 3 ili nione utekelezaji wake umefikia wapi.

CHETA, KAZOLE, MAGODANI, TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA

Cheta ni kitongoji kinachopatikana ndani ya kijiji cha Kazole kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Maendeleo huletwa na watu, watu wenyewe ndio sisi tukishirikiana na viongozi wetu ndipo tunaweza kupiga hatua chanya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio.

Ila wazo ili naona linapingana na uhalisia wa maisha ya wananchi na wakazi wa eneo la Cheta pamoja na viunga vyake.

Ikiwa imepita miezi michache ndani ya mwaka huu wa 2017 tayari zimeonekana alama za vijiti zinazo ashiria njia za uwekaji wa nguzo za umeme.

Alama izo zimetokea eneo la Vikindu zimepita eneo la Kazole mjini, Kazole shule ya msingi iliyopo mpakani na eneo la Hamidu na nguzo ya mwisho imeishia Kazole Magenge 20 eneo la njia panda ya kwenda kwa Bakhresa ambapo ndipo mpakani mwa Kazole na Cheta.

Sasa kuanzia hapo mpakani mwa Cheta na Kazole kwenda hadi mpakani mwa Cheta na Magodani hakuna alama yoyote inayo onyesha kuwa nguzo za umeme zitapita ili kwenda mpaka Magodani.

Cheta ipo ndani ya Kazole uku ikipakana na Magodani ila viongozi wa kazole kwa ujumla wamekuwa wakipasahau sana Cheta.

CHETA, KAZOLE, MAGODANI,  TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA
CHETA, KAZOLE, MAGODANI,  TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA

Baada ya uongozi wa Magodani kuchonga barabara yao kuanzia mpakani mwa Cheta kuelekea kwao ndipo Kazole wao walisimika alama za kuonyesha njia za nguzo za umeme zitakapo pita na wao wakaishia mpakani mwa Kazole na Cheta

Je Cheta inayoachwa katikati inaongozwa na akina nani?? Na je kama ina viongozi wake ivi wao wanatambulika upande wa Magodani au upande wa Kazole?? Wananchi wanataka kufahamu.

Kumbuka wakazi wote wa maeneo ya Mwasonga, Magodani, Cheta, Kazole na Vikindu wanategemea Barabara inayoanzia Vikindu hadi uko Mwasonga pamoja na maeneo mengine ambayo sikuyataja sasa je kama maendeleo na miundo mbinu vinawekwa mwanzoni mwa eneo na mwishoni bila kupaunganisha katikati je kunatengeneza kitugani jamani??

Wananchi wa Cheta wanataka maendelea ya kweli kwa vitendo nasio maendeleo ya kuongea mdomoni na kuwadanganya kwenye mikutano ya vijiji inayofanyika.

Wakazi wa Cheta wanataka Barabara safi, Shule ya msingi na ya Sekondari, Hospital, Soko, Umeme, Visima vya Maji masafi, Viwanja vya Michezo, Sehemu za ibada (Miskiti/Makanisa), Maziko nk.

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILIWAKO (BODY MASS INDEX BMI)

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILIWAKO
               (BODY MASS INDEX BMI)

Kanuni(BMI)=uzito ÷ (urefu)kipeo cha pili
                    [ Kg ÷ Meter ÷ Meter ]

BMI ikiwa chini ya 18.50 uzito wako upo chini kuliko kawaida (UNDER WEIGHT).

BMI ikianzia 18.50 hadi 24.99 wewe ni mwenye Afya njema kabisa (HEALTHY).

BMI ikianzia 25.00 hadi 29.99 wewe uzito umezidi (OVER WEIGHT) hivyo uzito wako na urefu wako haviendani kabisa sawa.

BMI ikianzia 30.00 na kuendelea, wewe ni mtu aliyepitiliza kabisa kiwango cha uzito na unaingia katika kundi la (OBESITY).

Tuangalie kwa mfano mimi Muta nina uzito wa Kg 52 na urefu wa Mita 1.65

         BMI ya Muta=52÷1.65÷1.65
                         BMI=19.100
Wanangu Diana Mutalemwa Juvenary pamoja na  Allen Mutalemwa Juvenary

Kwa mfano huo basi Muta yupo kwenye kundi salama maana BMI yake ni 19.100

   BAADHI YA MADHARA YA KUWA NA UZITO ULIOZIDI (BMI 25 NA KUENDELEA)

-Magonjwa/matatizo ya Ini na Figo
-Kisukari, Shinikizo la damu, Kiharusi, tatizo la Moyo na magonjwa mengine.
-Kutopumua vizuri wakati wa usingizi
-Kiwango cha juu cha mafuta mabaya
-Ugonjwa wa mifupa kama yabisi
-Matatizo ya hedhi kwa akinamama
-Upungufu wa nguvu za kiume nk.

HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MKOA WA PWANI, NI JUU YA KITUO CHA MABASI KUAMISHIWA MKURANGA

Wakazi wa Mwandege, Vikindu, Kazole, Cheta, Kisemvule, Mwanambaya, Jaribu, Kibiti, Ikwiriri na kwingineko kote kaeni mkao wa kupokea maendeleo makubwa saa na wakati wowote.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Wilaya za Temeke na Mkuranga kuangalia namna ya kupunguza msongamano uliopo katika eneo la Mbagala.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Moja ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na viongozi wa wilaya hizo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafua njia za kuondoa msongamano huo.

Amesema kwa sasa hakuna namna ambayo wataweza kuondoa msongamano huo zaidi ya kuhamishia kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini wilayani Mkuranga.

Waziri Mkuu amesema eneo la Mbagala kwa sasa lina msongamano mkubwa ambao ni lazima Serikali ichukue hatua za haraka za kuuondoa.
“Ikiwezekana mabasi ya mikoa ya kusini yaishie Mkuranga, hivyo shirikianeni kutafuta eneo la kujenga kituo kikubwa cha kisasa cha mabasi,” amesema.

Amesema kituo hicho watakachokijenga kiwe na uwezo wa kuhudumia mabasi yote yatokayo mikoa ya kusini na kituo cha Mbagala kiwe cha daladala za kawaida.

Pia Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kutawezesha kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.

Aidha Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kwenda kujadiliana katika vikao vya mabaraza ya Madiwani juu ya mkakati huo na kisha kumpelekea taarifa ifikapo Februari 15 mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga amesema wazo hilo ni zuri na wilaya yake ina maeneo ya kutosha kujenga miundombinu hiyo.

“Ni kweli wilaya ya Temeke imeelemewa kwa maana ya maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maendeleo na haina pa kupumulia zaidi ya Mkuranga , hivyo tupo tayari kushirikiana nao,” amesema.

Wakati huo huo, Bw. Sanga ameiomba Serikali itakapoanza awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi ufike hadi Mkuranga mjini badala ya kuishia Vikindu.

Amesema kwa sasa wilaya yake ina viwanda 67 ambavyo kati yake vipo vinavyofanya kazi na vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, hivyo mabasi hayo yatarahisisha usafiri kwa wafanyakazi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva amesema amefurahishwa sana na mawazo hayo ya kuhamisha kituo cha mabasi cha Mbagala kwani katika vitu vilivyokuwa vinamnyima usingizi ni pamoja na msongamano wa mabasi na wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo hilo.

Makonda na Sirro waitwa Mahakamani leo. Habari kamili iko hapa

Makonda na Sirro waitwa Mahakamani leo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam (ZPC), Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo (ZCO), Camilius Wambura, wamepelekewa barua za mwito za kuwataka wafike Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.

Viongozi hao wamepelekewa mwito huo kutokana na kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe dhidi yao.

Mbowe amefungua kesi hiyo kupinga Makonda kumtaja katika orodha yake ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na dawa za kulevya katika awamu ya pili na kumtaka afike katika Kituo Kikuu cha Polisi, Februari 10 mwaka huu, kwa ajili ya mahojiano.

Katika kesi hiyo Namba Moja ya Mwaka 2017, Mbowe pamoja na mambo mengine, anapinga mamlaka ya RC kumkamata kwa kile anachokiita kudhalilisha watu.

Kesi hiyo imepangwa kutajwa leo na itasikilizwa na jopo la majaji watatu, Sekieti Kihiyo ambaye ni kiongozi wa jopo hilo, akisaidiana na Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Kaday.

Mbowe anaiomba mahakama hiyo itamke kuwa vifungu vya Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa vinavyowapa mamlaka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuwakamata watu na kuwatia mbaroni viko kinyume cha Katiba.

Aidha, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, jana alifungua maombi mahakamani hapo akipinga kusudio la Kamanda Sirro la kumkamata kama hatajisalimisha katika kituo cha polisi kwa mahojiano.

Mahakama hiyo imetoa hati za mwito wa kufika mahakamani hapo kwa wadaiwa hao ambao ni Makonda, Sirro na Wambura. Hata hivyo, inadaiwa Kamanda Sirro alikataa kupokea mwito huo akielekeza kuwa hati hiyo ya mwito ipelekwe kwa Wambura.

Wadaiwa kukataa kusaini Kwa mujibu wa Ofisa wa mahakama, Yusuph Juma ambaye alipeleka mwito huo, alidai kuwa baada ya kuelekezwa na Kamanda Sirro kuwa ampelekee mwito huo Wambura, alipokwenda kwa Wambura, hakumkuta.

Juma alidai hati ya mwito wa mkuu wa mkoa alipoupeleka hakumkuta na kwamba wasaidizi wake nao walikataa kuusaini mwito huo.
Chanzo: HabariLeo

JE NAULI YA KUTOKA MBAGALA RANGI 3 HADI VIKINDU NI TSH 400 AU 500? SUMATRA TUNAOMBA UFAFANUZI

Mimi leo nayasema haya mbele yenu nyinyi wasafiri wenzangu nikiwa na ushaidi wa kutosha kabisa.

Magari yote yenye TLB ya kutoa huduma ya usafiri kutoka Temeke hadi Vikindu kupitia Kirwa Road pamoja na yale yote yenye TLB ya Mbagala Rangi tatu hadi Kisemvule, magari haya yamekuwa yakiwatoza abiria wao nauri kubwa kinyume na ile waliyopangiwa kwenye TLB zao.

Mpaka sasa unaposoma habari hii ndugu msomaji wangu nikwamba abiria anayetoka Mbagala rangi tatu hadi Vikindu anatozwa nauri ya Tsh 500 wakati TLB ya gari hilo inamtaka abiria atozwe Tsh 400 pekee.

Lakini pia wale wanaotoka Temeke moja kwa moja hadi Vikindu wao wanatakiwa kulipa Tsh 500 na wale wanaoishia Mbagala walipe 400 na wanao anzia Mbagala hadi Vikindu nao walipe 400 ila hawa wa Mbagala hadi Vikindu hutozwa Tsh 500

Kingine nikwamba unakuta kwenye Tiketi zao wameacha baadhi ya vituo vikubwa, mfano ulio hai tazama tiketi za magari aya utajua ninachokizungumzia, magari aya TLB zake imeandikwa Temeke - Vikindu= 500
Temeke - Mb/Rangi 3= 400
Mb/Rangi 3 - Vikindu =400
Mwanafunzi ni Tsh 200

Ila wao kwenye tiketi zao wameandika
Temeke - Vikindu= 500
Temeke - Mb/Rangi 3= 400
Mwanafunzi 200

Swali ni je kwanini Mbagala hawakuiandika kwenye tiketi zao??

Na kila abilia wakilala mika hawapati msaada, na wakijaribu kuwahoji makondakta wanasema eti Vikindu ipo mkoa mwingine kwaiyo iyo ndio sababu kubwa.

Viongozi wa dini na wamiliki wa hoteli na migahawa, wanaweza kuwa na taarifa zitakazoisaidia polisi

Mbowe, Gwajima, Manji mkononi mwa Makonda.

Baada ya awamu ya kwanza kuwalenga wasanii, jana alitaja orodha ya watu 65 iliyohusisha wanasiasa, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, viongozi wa dini na wamiliki wa hoteli na migahawa, akisema wanaweza kuwa na taarifa zitakazoisaidia polisi kuwabaini wauzaji wa dawa hizo.

Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, zaidi ingia hapa

Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, asema si kazi ya Makonda pekee

Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya.

Asema si kazi ya Makonda pekee. Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.

Rais Magufuli amesema anamuomba Jaji Mkuu asizicheleweshe kesi za madawa ya kulevya kwani kuna mtuhumiwa mkubwa wa Dawa za Kulevya anashikiliwa Lindi bila ya kufikishwa Mahakamani.

Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP. Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni.

MABADILIKO YA BEI ZA UMEME YALIYOTANGAZWA LEO NA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA), FELIX NGAMLAGOSI.

MABADILIKO YA BEI ZA UMEME YALIYOTANGAZWA LEO NA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA), FELIX NGAMLAGOSI.
Bei za umeme zimepanda kwa 8.5% badala ya 18.19% iliyopendekezwa na TANESCO.

Ongezeko la bei ya huduma za umeme limetokana na kuzidi kwa gharama za uzalishaji wake.

Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa 5.7% ya bei ya umeme.

Ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.
Kundi la TIb linalohusisha viwanda vidogo,mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

Bei hizo zitaanza kutumika Januari Mosi mwaka 2017.

TANESCO inatarajia kufanya maboresho ya msongo wa umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme.

IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO).

Ifikapo 2017 vituo vyote vya Tv viwe na wakalimani wa lugha ya alama

Katika kuadhimisha ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameagiza vituo vyote vya runinga nchini ifikapo Machi mwaka 2017, kuweka wakalimani wa lugha za alama katika taarifa za habari na matukio ili watu wenye ulemavu wa kusikia wapate habari .

“Ifikapo 2017 vituo vyote vya Tv viwe na wakalimani wa lugha ya alama ili kutekeleza matakwa ya sheria namba 9 hasa katika habari ili walemavu wafuatilie matukio na habari bila ya kuachwa nyuma,” amesema.

Pia amewataka watendaji wa serikali kupanga mipango itakayojibu mahitaji ya watu wenye ulemavu nchini.

Pia ameagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwasimamia waganga wakuu kuagiza mafuta ya kuzuia athari za mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

“Natoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini wawasimamie waganga wakuu wanapoagiza dawa MSD waagize na mafuta ya kukinga mionzi ya jua dhidi ya ngozi za maalbino, ili kundi hilo lipate mafuta hayo kwa uraisi. MSD pia ijumuishe mafuta ya ngozi katika orodha ya dawa inazoagiza,” alisema.


Pia Mhagama amewaagiza watendaji wa serikali kuunda kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya kata ili ziratibu changamoto za walemavu kwa ajili ya serikali kutenga bajeti ya kutatua changamoto hizo.

“Watendaji wa serikali waunde kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya mtaa ili ziweze kujadili changamoto za watu wenye ulemavu. Kamati hizi ziundwe ili bajeti zake ziingie katika bajeti kuu ya serikali,” alisema.

Kuhusu walemavu kupewa msamaha wa matibabu, amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya afya inandaa utaratibu wa walemavu kupata huduma ya afya bure bila kubaguliwa.

“Tumekaa na wizara ya afya kuandaa taratibu za walemavu kupata huduma bila kubaguliwa, hivi karibuni changamoto yenu itakwisha,” alisema.

Aidha, amevitaka vyama vya watu wenye ulemavu nchini kuadhimisha siku ya walemavu duniani katika mikoa yote ili kuongeza uelewa kwa wananchi na walemavu kupatiwa stahiki zao.

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi. Lakini wanapotambua kwamba wameshaoa hushangaa sana na huumia na kusema wanaume wote ni mbwa tu. 

Wanaume sio mbwa ni wao wenyewe ndio wameshindwa kufanya uchunguzi. 

Tulishaambiwa kwenye kila mafanikio ya Mwanaume nyuma yake Kuna mwanamke. Na wewe unataka Mwanaume mwenye mafanikio unategemea nini???

Huyo sio mumeo mtarajiwa huyo ni mume wa mtu Fulani Ni agharabu sana kukutana  na Mwanaume anayejiweza akawa single, either uwe shareholder au unyanganye share ya mwanamke mwenzio kitu ambacho sio busara.

Mume wako yupo anahangaika kutoka kimaisha anapigania ndoto zake. Huenda yuko shule, shambani, dukani au anabeti kimsingi yupo anapigania kutoka Kimaisha.

Anakusubiri tu wewe umpe support na back-up ya kutosha mtafute huyo uanze nae chini na sio kukimbilia waume za watu.

Bunge la Tanzania limeridhia msimamo wa Serikali ya Tanzania wa kutokusaini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi (EPA)

Bunge la Tanzania limeridhia msimamo wa Serikali ya Tanzania wa kutokusaini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi (EPA) baina ya nchi za jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na umoja wa ulaya(EU).

My take:
Nawashukuru sana Wabunge wa Tanzania kwa kuweka Taifa kwanza mbele, na ninashukuru Edward Lowassa na Sumaye waliotia nanga Dodoma kuwafunda wabunge wa UKAWA, matunda yanaonekana.

Naishauri Serikali iache kisainia Mikataba Ikulu. Ni vyema Mikataba yote iwe inapitia bungeni kwa Masilahi mapana ya nchi. Naamini kama Serikali ingekuwa na utaratibu wa kupitisha Mikataba Bungeni, sasa hivi tungekuwa tumeona manufaa ya Madini, gesi na Mafuta.

Msikilize mhe Tundu Lisu akiwasha moto Bungeni juu ya uhuru wa habari nchini.

Kiukweli kabisa tukiachilia mambo ya ushabiki wa vyama, mimi binafsi waga namkubali sana mhe.Tundu Lisu, nimtu anaejielewa kila mda yaani yuko smart antime.

Na leo alikuwa akichangia juu ya mswada wa uhuru wa habari palikuwa hapatoshi bungeni.
===>> BOFYA HAPA KUMSIKILIZA <<===


Bunge laupitisha Muswada wa Huduma za Habari tayari kusainiwa na Rais kuwa sheria. Makosa ya Mwandishi kutokigharimu chombo chake.

Bunge laupitisha Muswada wa Huduma za Habari tayari kusainiwa na Rais kuwa sheria. Makosa ya Mwandishi kutokigharimu chombo chake.
Rais Magufuli jana alisema ukifika mezani kwake hautafikisha dakika bila kusainiwa.

Bunge leo limeupitisha Muswada wa Huduma za Habari tayari kusainiwa na Rais ili kuwa sheria kamili. Katika muswada huo makosa ya Mwandishi hayatagharimu chombo chake cha habari.

Mswada huo uliwasilishwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kisha wabunge wakaanza kuujadili. Muswada wa sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016 umejadiliwa kwa siku mbili.

Jana Rais Magufuli wakati akifanya mahojiano na wahariri wa vyombo vya habari alisema ukifika mezani kwake hautafikisha dakika bila kusainiwa.

RC GAMBO APOKEA MSAADA WA BATI 500 NA MIFUKO YA SARUJI 500

Nteghenjwa Hosseah - Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Arusha.

Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo, Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko 100 ya saruji na mabati 100  kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.

Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil - Jiangsu Joint Venture Ltd, inayojenga barabara ya Sakina - Tengeru Km 14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.

"Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto mbalimbali kwa jamii ".


Naye Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Bw. Xie alisema kampuni yao imeona umuhimu wa kuchangia jamii kwani wao ni wajenzi wa barabara na wanastahili kurejesha faida kwa jamii inayowazunguka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro alimshukuru Gambo kwa msaada huo na kusisitiza kuwa mifuko hiyo 100 ya saruji pamoja na bati 100 zitasaidia ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa Kata ya Muriet Jijini Arusha.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru kwa msaada huo utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na kukamilika ndani ya miezi miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha Kituo kinajengwa katia ubora unaostahili.


Katika  makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na wabunge wa Viti maalum wanawake Mkoa wa Arusha, Catherine Magige na Aminah Mollel walitoa rai kwa nyakati tofauti kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumuunga mkono Mhe. Gambo pamoja na Serikali ili kuwezesha maendeleo kusonga mbele.

Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top