Tanzania na Uganda zimeanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka katika nchi ya Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola za Kimarekani bilioni nne.
Makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo yalifikiwa na marais wa nchi hizo Dr,John Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda walipokutana jijini Arusha wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mawaziri wa sekta zinazohusiana na nishati,makatibu wakuu na watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi za Tanzania na Uganda wamekutana jijini Arusha na kusaini makubaliano ya kuanza kwa mchakato ambao waziri wa nishati wa Uganda Bi.Irine Liuloni amesema mradi huo utaongeza chachu ya uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki .
Aidha viongozi hao wamesema kitakachofuata baada ya hatua hiyo ni taratibu za ndani za serikali za Tanzania na Uganda na kwamba mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya kimataifa ya uchimbaji wa mafuta ya total unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2017.
Kama mradi huo utakamilika na kuanza uzalishaji unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na ajira kwa wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Post a Comment