SERIKALI INADAIWA 28 BILLIONS NA HOSPITAL MBALIMBALI ZA NJE YA NCHI

Serikali inadaiwa shilingi bilioni 28 na Hospitali mbalimbali za nje ya nchi kutokana na watu waliokwenda kupata huduma ya matibabu yakiwemo ya moyo huku watoto zaidi ya 500 wakihitaji huduma ya upasuaji.

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia,watoto na wazee Mh.Ummy Mwalimu ametoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea msaada wa zaidi ya sh.Milioni mia mbili kwa ajili ya kusaidia watoto 101 kupata huduma ya upasuaji wa moyo na kuongeza kuwa kutibu mgonjwa mmoja nje ni milioni 16 lakini kwa hapa nchini ni sh Milioni 4 tu.


Hafla hiyo ya kupokea msaada imefanyika taasisi ya moyo iliyopo hospitali ya taifa Muhimbili  daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Prof Mohamed Janabi, amesema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni uhaba wa damu kwani wakati mwingine huwezi kufanya upasuaji kama huna akiba ya damu pamoja na sasilimali fedha kutokana na idadi kubwa ya wanaofika kupata huduma hawana uwezo  kifedha.

Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wameshapatiwa huduma ya upasuaji na wanaosubiri huduma hiyo wameiomba serikali kuzisogeza mikoani kwani wanatoka mbali tena kwa gharama kubwa kufuata huduma hiyo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top