Hofu yazidi kutanda baada ya watu 80 kupoteza maisha, zaidi bofya hapa

Wizara ya afya ya Afghanistan imesema takriban watu themanini wameuawa na zaidi ya wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye mji mkuu Kabul. Baadhi ya taarifa zinasema kulikuwa na milipuko miwili.

Shambulio hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa ukatili.

Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top