wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba zaidi bofya hapa

Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed a.k.a Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba. 

Mwigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa filamu ambao wanafanya vizuri kwa sasa, amedai kama wasanii wakiamua kufanya kazi kwa bidii basi kila kitu kinawezekana. 

“Pengo la marehemu Kanumba litazibika tu ingawa najua tobo la panya huwezi kuziba na mkate ila tutajitahidi kuziba,” Gabo alimjibu shabiki katika Kikaango cha EATV. 

Aliongea,”Niwashauri watu wawe makini kwenye nidhamu, wawe makini kwenye elimu na pia wasikate tamaa katika mambo wanayofanya”  Mwigizaji huyo amemtaja Single Mtambalike kuwa ndiye mwigizaji wake bora kwa sasa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top