Jifunze zaidi kwa kupitia ujumbe uliopo hapo juu
Wanawake wanapenda harusi na wanachukia ndoa na wanaume wanapenda ndoa na wanachukia harusi, harusi ni sherehe ya siku moja na ndoa ni mkataba ambalo lengo lake ni hudumu milele.
Wengi walipenda harusi ila walipoingia kwenye ndoa hawakuwa na furaha sababu walipenda zaidi kuvaa gauni/suti za harusi kuliko kuwa tayari kuyavaa majukumu ya ndoa na uwajibikaji.
Ndoa nyingi za mbwembwe huwa na mwisho mchungu na hasa pale wahusika walioingia kwenye ndoa kwa hitaji moja la kuoa/kuolewa sababu ya msukumo wa wazazi au pesa za muda mfupi au kushika mimba na kuwa kiunganishi cha ndoa.
Wanawake/Wanaume wanapenda kuzaa ila wanachukia malezi na ndio maana unakuta msichana mwenye mtoto ana miaka 23 ila mtoto wake analelewa na mama yake na yeye anakula ujana sababu hawezi kulea mtoto wake mwenyewe.
Wanaume wengi wanajua kuzalisha ila kutunza hawawezi na akifanikiwa kutunza jua hawezi kulea mtoto.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kulea mtoto na kutunza mtoto ,kutunza mtoto ni kazi rahisi sana sababu unamtumia mtoto pesa ya chakula ,mavazi pamoja na karo ya shule.
Picha kutoka maktaba
Ila kumpa mtoto malezi ni ile hali ya kutengeneza chemistry nzuri na mtoto kwa uwepo wako na kumuandaa kisaikolojia kujua umuhimu wa baba kwa kuona na kusikia.
Ndoa nyingi zilizofungwa kwa harusi ndio zinazo ongoza kwa kuvunjika na moja ya sababu ya kuvunjika kwa ndoa hizo ni watu kupenda zaidi harusi kuliko kuithamini ndoa.
Mtu anafikilia zaidi honey moon badala ya kutafakari jinsi ya kuboresha ndoa na kuwa na kizazi chenye maisha bora na matamu.
Kuoa au kuolewa na mtu anayekupenda kwa dhati ya moyo wake ni baraka kubwa mno ambayo anakuwa ameiandaa Mungu wetu muumba mbingu na nchi.
Kama umeoa au umeolewa basi mpende na pia muheshimu sana mwenzi wako maana ujui kitakacho kutokea mda mfupi ujao kutoka sasa, usije ukafa ukiwa na dhambi ya kumdharau mumeo/mkeo.
Jifunze zaidi kwa kupitia ujumbe uliopo hapo chini.
Post a Comment