Watumishi wa umma Zanzibar kuwasilisha mali zao kwenye tume ya daadili

Serikali ya Mapinduizi ya Zanzibar imewataka viongozi wote wa umma kuwasilisha mali na madeni yao katika tume mpya ya maadili ya viongzoi wa umma katika kipndi cha mwaka wa fedha 2016/2017 ikiwa ni miongozi mwasheria mpya inayoanza kazi kiswani Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nchi ofisi ya rais katiba, sheria, utumishia wa umma na utawala bora Mhe Haroun Ali Suleiamn wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea kisiwani Zanzibar ambapo amesema hatua hiyo ina lengo la serikali kuweka uwazi na viongozi kuwajibika kwa wananchi ambo ndio waajiri wa viongozi hao.

Wizara hiyo ambayo ni mpya na imechanganywa na taasisi mbalimbali za jamii ambapo Mhe Haroun aliliambia baraza hilo mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta zake zikiwemo za sheria, uthibiti wa fedha na masuala ya mahakama ambapo kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali ya baraza Mhe Mwantanga Mbaraka ameitaka wizara kuchuka hatua za kufuatilia matumizi ya fedha ndani ya taasisi za serikali ambapo kuna tafauti kubwa ya matumizi ya Unguja na Pemba nao baadhi ya wajumbe waliochangia akiwemo Mhe Simai Said Mwakilishi wa Tunguu ambaye alitaka wizara hiyo kupambana kikamilifu na suala la madawa ya kulevya.

Wajumbe wanaendelea kuijadili bajeti ya wizara hiyo ambayo ni moja ya wizara ambayo inagusa hisia za jamii kutokana na taasisi zote zinagusa maisha ya wafanyakazi na wananchi zimo katika wizara hiyo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top