Kamati ya Uchaguzi ya kablu ya Yanga leo imetengaza tarehe rasmi ya uchaguzi wa klabu hiyo kuwa Juni 11,huku ikisisitiza TFF na BMT wakae kama waangalizi katika uchaguzi huo.
Akiongea na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Baraka Deus amesema kuwa kuwa awataki maslai ya timu hiyo yasimamiwe na watu walionje ya timu hiyo.
Amesema kuwa Juni 2hadi 3 wagombea watatakiwa kuchukua na kuzirejesha ambapo Juni 4 kikao cha mchujo wa awali kitakaa na Juni 5 itakuwa siku ya kupokea mapingamizi.
Ameongeza kuwa Juni 6 kamati ya uchaguzi watapitia mapingamizi yote na Juni 7 mpaka 10 itakuwa siku za kampeni kwa wagombea,Jumamosi Juni 11 itakuwa siku ya uchaguzi na jumapili juni 12 matokeo yatatangazwa na mwenyekiti wa Yanga atakuwa amepatikana.
Post a Comment