Wakati wa kijana kujipanga ni sasa usisubili baadae, bofya hapa kujua zaidi

WAKATI WA KIJANA KUJIPANGA NI SASA USISUBILI BAADAE
Habari za leo ndugu yangu, nimatumaini yangu kuwa utakuwa umevutiwa na habari hii ambayo inalenga kuwakumbusha vijana wa kiume na vijana wa kike kujipanga kabla ya wao kuoa au kuolewa.

Kwa leo nitazungumzia faida na hasara kwa vijana ambao watakuwa wamejipanga kabla ya kuoa au kuolewa.

Naomba nianze kwa kusema neno moja kwenu vijana wa kiume, kwamba ukisikia kijana anasema kuwa anataka kuoa akilini mwako tambua kwamba kijana huyo anaenda kutengeneza mfumo ndani ya mfumo.

Kutengeneza mfumo ni nini??
Kutengeneza mfumo ni kitendo cha kufanya jambo moja ndani ya jambo lingine, kwa lugha ambayo utaweza kuelewa kwa haraka zaidi nikwamba "wewe ulikuwaunaishi mwenywe kabla ya kuoa, huo ndio mfumo wa kwanza na ukisha amua kuoa huo nao unakuwa mfumo mwingine wa pili.

Kwaiyo kama kuoa ni kutengeneza mfumo ndani ya mfumo mwingine ni vyema kujipanga vyema kuakikisha kuwa unaweza kuimiliki mifumo yote miwili.

Unaweza kuimiliki mifumo yote kwa kujiwekea utaratibu juu ya maisha yako,  vijana wengi wanapenda kuoa pasipo kuwa na mipango ya maisha yao jambo ambalo linakuja kuwaletea utata na wake zao kipindi cha ndoa zao.

Ukiwa bado ujaoa na ukajiwekea utaratibu mzuri wa kufanya mambo yako ya maendeleo utakuwa na nafasi nzuri sana ya kufanikiwa kimaisha, lakini endapo ukishindwa kuyafanya hayo yote kipindi bado uko peke yako na ukajidanganya ya kwamba utayafanya mambo yako kwa kushirikiana na mke wako hapo utakuwa umepotea kabisaaa.

Familia inaongozwa na baba, mama nafasi yake ni yapili kwaiyo majukumu yote ya kutafuta pesa yanakuwa juu yako wewe kijana wa kiume/mwanaume, mwanamke yeye ni kutumia kile unachokileta hapo nyumbani.

Japo sikuizi akina mama nao wanafanya kazi zao na kulipwa mishahara, ila ata kama anafanya kazi na kulipwa unatakiwa ufahamu ya kwamba pesa ya mwanamke huwezi kuipangia majukumu wewe mwanaume.

Usioe mwanamke kama ujawa na plani nzuri juu ya kuendesha familia yako, kumbuka yakwamba kipindi uko peke yako ulikuwa unatumia Tsh 50,000/= kwa mwezi, ukisha kuwa na mke utatumia zaidi ya 100,000/= je ukija kuongeza na mtoto wa kwanza utatumia kiasi gani?

Zilizotangulia zilikuwa nifaida za kujipanga kabla ya kuoa au kuolewa, na kwaupande wa hasara nikwamba ukishindwa kujipanga mapema hautaweza kujipanga ukisha oa au kuolewa.

Je kama utakuwa ujajipanga wakati wa ubachera utaweza kuyaendesha maisha yako pamoja na familia yako?. Naomba nimalizie kwa kusema yakwamba " Wakati wa kujipanga ni pale ambapo unakuwa ujawa na majukumu makubwa"

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top