HUU NI WIZI WA KIWANGO CHA PHD. HEKARI 1 YA ARDHI, BILIONI MOJA??

HUU NI WIZI WA KIWANGO CHA PHD.
HEKARI 1 YA ARDHI, BILIONI MOJA??

Nimepitia hii ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya NSSF.

Kwamba shirika hilo la umma lilitumia TZS 250,787,041,800 (Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Milioni Mia Saba) kununua ekari Mia tatu za ardhi katika mji wa Kigamboni. Kwa hiyo kila ekari moja ilinunuliwa kwa TZS 835,956,806 (Shilingi Milioni mia nane thelathini na tano).

Kama kuna watu wamesomea wizi kwa kiwango cha PhD basi hapa Tanzania tunaongoza. Yaani ardhi ya Kigamboni inauzwa ekari moja kwa takribani shilingi milioni elfu moja (Bilioni 1)! Pesa za wanachama wa NSSF! Pesa za umma! Kama ni kwenye mpira wa leo (soka) basi aliyetufundisha ni Lionel Messi!

Na Jana nimemsikia JPM anasema meli zaidi ya 60 zilizoingia kwenye Pwani ya Tanzania (Bandarini) zilipotea katika mazingira ya kiutatanishi. Nikajisemea kimoyomoyo,"huwenda ziliwekewa matairi na sasa ni daladala". Yani hata meli inapotea! (Yaani meli nzima hailipi kodi na haijulikani iliko tena). Huwenda ziliposhusha mizigo zilizama!

Tatizo linalokabili taifa hili ni kukosa nguvu za kimifumo za kuongoza taifa.

Na hadi sasa sijaona juhudi zozote za kujenga mifumo yenye nguvu hapa Tanzania. Baada ya miaka 10, tutakuwa tunalia na kuumizwa na matatizo yale yale.

Shikamoo wale wote waliopiga Bilioni 200 za ununuzi feki wa ardhi. Saluti kwenu mliozamisha meli 60. Nyinyi ni vichwa!

Kwa mtindo huo hatuwezi kuendelea tutabaki tu mtu mmoja ambaye ni Raisi wetu peke yake atumbue majipu lazima tusaidiane au tumsaidie Raisi wetu mpendwa Magufuli kutumbua majipu yaliyokwisha kuiva.

Endelea kuwanasi tukujuze zaidi kupitia hapa hapa kwenye tovuti ya Mikoa Yetu inayopatikana kupitia link ifuatayo hapa mbele:> http://mikoayetu.blogspot.com


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top