MINI SHOP CHETA

Mini Shop Cheta au Duka Dogo
Mini Shop Cheta logo
Mini Shop logo
Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.
Mini Shop Cheta
Mini Shop Cheta
Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.

Mini Shop Cheta Management
Mini Shop Cheta Management
Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. bidhaa izo zipo chini ya picha hii.
Mini Shop Cheta Map
Mini Shop Cheta Map
Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara
Chumvi
Mchele
Sukali
Mini Shop Cheta Manager
Mini Shop Cheta Manager

Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari
Vichongeo
Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Mini Shop Cheta Management finishing
Mini Shop Cheta Management finishing
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka
Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria
Maharage ya Njano
Mini Shop Cheta before plaster
Mini Shop Cheta before plaster

Maharage ya Kombati
Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.
Mini Shop Cheta map Foundation
Mini Shop Cheta map Foundation
Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop Cheta tukuhudumie leo.

NYUMBA PAMOJA NA FREMU ZA BIASHARA ZINAUZWA

NYUMBA PAMOJA NA FREMU ZA BIASHARA ZINAUZWA

Nyumba hii ina idadi ya vyumba vitano (5) ambavyo unaweza kuvitumia kwenye matumizi yako binafsi kulingana na jinsi unavyotaka kutumia sehemu ya vyumba ivyo.
Cheta kwa Kijonjo

ipo karibu na barabara kuu ya serikari, kwaiyo inafaa sana kwa biashara pamoja na makazi ya kawaida tu ya kila siku kama kulala pamoja na huduma zingine.
Cheta kwa Kijonjo.

tayari imeisha fanyiwa wireling (mfumo wa umeme upotayari) kinachosubiliwa ni umeme kuwashwa tu basi alafu matumizi yaanze.
Cheta kwa Kijonjo frem

Kuhusu huduma ya maji ondoa shaka maana kisima kimechimbwa nyuma ya fremu/nyumba hii, pia eneo iloilo kuna huduma ya tofari, mchanga, cement, kokoto, nk.
Cheta kwa Kijonjo house

Nyumba hii au frem hii, ipo kijiji cha Kazole kitongoji cha Cheta kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. 

Bei ni tsh 24,000,000/- (millions ishirini na nne) pia mazungumzo yapo.


Mawasiliano:
0659 91 9292







KAMA KWELI UNATAKA KUFANYA BIASHARA PITIA HAPA

Mpenzi msomaji wa makala hii, napenda nikwambie kitu kwamba siku izi watu wengi wanapenda kuanzisha biashara zao binafsi uku lengo lao kuu nikuachana na kuajiliwa kisha wajiajiri wenyewe na kujipatia kipato kupitia biashara zao walizo zianzisha.

Biashara za kufanya ziponyingi sana hapa duniani,ambazo ukizisimamia vizuri zinakutimizia marengo yako.

Mini Shop_Cheta kwa wakala_Mutalemwa

Mbali ya kwamba biashara nyingi zenye faida ya haraka ni zile biashara ambazo zina madhara makubwa kwa afya wa wanadamu mfano waweza kuwa Sigara, Pombe, madawa ya kulevya nk.

Ila zipo biashara ambazo nazo zinakuwa na faida japo kuwa inapatikana taratibu na uchukua mda mrefu kidogo kuonekana tofauti na biasha nilizo tangulia kuzitaja hapo juu.

Biashara izo ni pamoja na Unga wa Sembe, Sukari, mafuta ya kula, Pipi, jojo, soda, maji, madaftari, karamu, nk. Sasa basi, ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yako yoyote ile utakayokuwa umeichagua kuianzisha unatakiwa kuwa na mipango mazubuti juu ya usimamizi na uendeshaji wa biashara yako.

Mini Shop+Cheta+kwa wakala+Mutalemwa

Mipango iyo nipamoja na kujua namna ya kutenganisha faida na pesa ya mtaji, kuweza kujua namna ya kuendesha mfumo mzima wa mauzo pamoja na manunuzi, kulipa mishahara nk.

Angalizo, huwezi kufanya biashara bila kumbukumbu, biashara yoyote ile inahitaji utunzaji wa kumbukumbu, usipoweza kipengele hiki basi jua kabisa wewe huwezi kufanya biashara yenye tija, bali unaweza kufanya biashara ya mazoea tu basi. Kujaribu sio kushindwa ebu anza leo uone miujiza ya biashara.

Viwanja vinauzwa kwa bei nafuu sana eneo la Cheta Kazole

Viwanja vinauzwa kwa bei nafuu sana eneo la Cheta_Kazole kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani (Mji unaokua).
          SIFA ZA VIWANJA HIVI
1. Vyote vipo eneo la tambarale, ni umbali wa Futi 320 sawa na Mita 97.55 kutokaka barabara kuu ya serikali.

2. Mchanga unaweza kuchimba kiwanjani mwako hapo hapo.

3. Bomba la maji ya kutumia limepita katikati ya barabara ya mtaa inayopita vilipo viwanja hivi.

4. Viwanja hivi vina urefu wa Futi 50 na upana wa Futi 40 kwa kila kiwanja ikiwa ni sawa na Mita 15.25 kwa mita 12.20

5. Ukubwa wa barabara ya mtaa inayo anzia kwenye barabara kuu ya serikali ina urefu wa Futi 320 na upana wa Futi 16.5 sawa na Mita 97.55 kwa mita 5.

Na ile barabara ya mtaa inayopita viwanjani hapo ina upana wa Futi 10 sawa na Mita 3.5, Pia kuna Futi 2 sawa na Mita 0.60  Zinazotenganisha eneo linalouzwa na eneo la mmiriki.

6. Huduma ya vifaa vya ujenzi kama, Cement, Nondo, Tofari, Mchanga, Kokoto, Maji, vyote vinapatikana jirani kabisa na viwanja hivi vilipo.

Vipo viwanja vinne (4) na kila kiwanja kimoja kinauzwa kwa Tsh. 1.3M (Million 1 na laki 3).
Maongezi yapo kwenye uitaji.

Pia unaweza kulipia kiwanja chako kwa hawamu mbili tu. 

Wote karibuni sana.
Mwenye viwanja naitwa Mutalemwa
Tuwasiliane kupitia 0659 919 292


MAELEZO KUHUSU UMBALI/NAULI
Viwanja hivi vinafikika kwa njia 3 za usafiri.

1. Vikindu kuna stendi ya magari yanayokwenda Kazole magenge 20 na mengine yanakwenda Magodani pia ziko pikipiki (Boda boda).

Kama ukipanda magari yanayoishia Kazole magenge 20 nauri ni Tsh 500 ambapo umbali wa Vikindu to Kazole magenge 20 ni 5.5KM.

Ukishuka hapo kazole utalazimika kutembea umbali wa 2.6KM au kuchukua pikipiki hapo kazole  hadi kufika viwanjani hapo kwa Tsh 1,000

Ila ukipanda magari yanayo kwenda mpaka Magodani nauri yake ni Tsh 1,000 ambapo umbali wa kutoka Vikindu to Cheta kwenye ivyo viwanja ni 8.1KM.

2. Usafiri wa pikipiki kutoka Vikindu to Cheta kwenye viwanja ni Tsh. 3,000

3. Unaweza kutembea kwa mguu kutoka Vikindu hadi Cheta kwenye viwanja hivi kwa mda wa dakika 50-60

Tuwasiliane kupitia 0659 91 9292 au 0787 63 7571

Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu

Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani na Kilongoni hadi Vikindu
inayopitia Cheta, Kazole kisha kuunganisha kwenye barabara kuu ya rami inayoenda mikoa ya kusini.

Aliyasema haya kwenye mkutano wake uliofanyikia tarehe 03/11/2017 eneo la Magodani kisha kuumalizia Kazole,  ambapo alisema tayari barabara hii ya kutoka Vikindu hadi Magodani kupitia Kazole na Cheta tayari imeisha wekwa kwenye bajeti na itatengenezwa mda sio mrefu.
Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu
Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu
Mbali na hili swala la barabara pia aliongerea kuhusu watu walio uziwa viwanja kwenye eneo la Hamidu kisha baadae wakaja kuvunjiwa nyumba na kunyang'anywa viwanja vyao.

Ambapo alisema atalishugulikia swala hilo baada ya kuwapata walioshiriki kuwauzia raia viwanja hivyo kutoka kwenye eneo la muwekezaji Hamidu.

Kuhusu swala la barabara hii ya Magodani kupitia Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu nitarudi baada ya miezi mitatu 3 ili nione utekelezaji wake umefikia wapi.

CHETA, KAZOLE, MAGODANI, TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA

Cheta ni kitongoji kinachopatikana ndani ya kijiji cha Kazole kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Maendeleo huletwa na watu, watu wenyewe ndio sisi tukishirikiana na viongozi wetu ndipo tunaweza kupiga hatua chanya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio.

Ila wazo ili naona linapingana na uhalisia wa maisha ya wananchi na wakazi wa eneo la Cheta pamoja na viunga vyake.

Ikiwa imepita miezi michache ndani ya mwaka huu wa 2017 tayari zimeonekana alama za vijiti zinazo ashiria njia za uwekaji wa nguzo za umeme.

Alama izo zimetokea eneo la Vikindu zimepita eneo la Kazole mjini, Kazole shule ya msingi iliyopo mpakani na eneo la Hamidu na nguzo ya mwisho imeishia Kazole Magenge 20 eneo la njia panda ya kwenda kwa Bakhresa ambapo ndipo mpakani mwa Kazole na Cheta.

Sasa kuanzia hapo mpakani mwa Cheta na Kazole kwenda hadi mpakani mwa Cheta na Magodani hakuna alama yoyote inayo onyesha kuwa nguzo za umeme zitapita ili kwenda mpaka Magodani.

Cheta ipo ndani ya Kazole uku ikipakana na Magodani ila viongozi wa kazole kwa ujumla wamekuwa wakipasahau sana Cheta.

CHETA, KAZOLE, MAGODANI,  TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA
CHETA, KAZOLE, MAGODANI,  TUNATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA

Baada ya uongozi wa Magodani kuchonga barabara yao kuanzia mpakani mwa Cheta kuelekea kwao ndipo Kazole wao walisimika alama za kuonyesha njia za nguzo za umeme zitakapo pita na wao wakaishia mpakani mwa Kazole na Cheta

Je Cheta inayoachwa katikati inaongozwa na akina nani?? Na je kama ina viongozi wake ivi wao wanatambulika upande wa Magodani au upande wa Kazole?? Wananchi wanataka kufahamu.

Kumbuka wakazi wote wa maeneo ya Mwasonga, Magodani, Cheta, Kazole na Vikindu wanategemea Barabara inayoanzia Vikindu hadi uko Mwasonga pamoja na maeneo mengine ambayo sikuyataja sasa je kama maendeleo na miundo mbinu vinawekwa mwanzoni mwa eneo na mwishoni bila kupaunganisha katikati je kunatengeneza kitugani jamani??

Wananchi wa Cheta wanataka maendelea ya kweli kwa vitendo nasio maendeleo ya kuongea mdomoni na kuwadanganya kwenye mikutano ya vijiji inayofanyika.

Wakazi wa Cheta wanataka Barabara safi, Shule ya msingi na ya Sekondari, Hospital, Soko, Umeme, Visima vya Maji masafi, Viwanja vya Michezo, Sehemu za ibada (Miskiti/Makanisa), Maziko nk.

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILIWAKO (BODY MASS INDEX BMI)

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILIWAKO
               (BODY MASS INDEX BMI)

Kanuni(BMI)=uzito ÷ (urefu)kipeo cha pili
                    [ Kg ÷ Meter ÷ Meter ]

BMI ikiwa chini ya 18.50 uzito wako upo chini kuliko kawaida (UNDER WEIGHT).

BMI ikianzia 18.50 hadi 24.99 wewe ni mwenye Afya njema kabisa (HEALTHY).

BMI ikianzia 25.00 hadi 29.99 wewe uzito umezidi (OVER WEIGHT) hivyo uzito wako na urefu wako haviendani kabisa sawa.

BMI ikianzia 30.00 na kuendelea, wewe ni mtu aliyepitiliza kabisa kiwango cha uzito na unaingia katika kundi la (OBESITY).

Tuangalie kwa mfano mimi Muta nina uzito wa Kg 52 na urefu wa Mita 1.65

         BMI ya Muta=52÷1.65÷1.65
                         BMI=19.100
Wanangu Diana Mutalemwa Juvenary pamoja na  Allen Mutalemwa Juvenary

Kwa mfano huo basi Muta yupo kwenye kundi salama maana BMI yake ni 19.100

   BAADHI YA MADHARA YA KUWA NA UZITO ULIOZIDI (BMI 25 NA KUENDELEA)

-Magonjwa/matatizo ya Ini na Figo
-Kisukari, Shinikizo la damu, Kiharusi, tatizo la Moyo na magonjwa mengine.
-Kutopumua vizuri wakati wa usingizi
-Kiwango cha juu cha mafuta mabaya
-Ugonjwa wa mifupa kama yabisi
-Matatizo ya hedhi kwa akinamama
-Upungufu wa nguvu za kiume nk.

Kama wewe ni mpenzi na mshabiki wa msanii Diamond Platinum, ebuingia hapa uone kufuru

Pete na cheni mpya za Diamond Platnumz alizozivaa kwa wakati mmoja zina thamani ya shilingi milioni 158!

Hitmaker huyo wa Marry You amepost Instagram picha mbili zikionesha madini hayo kwa kile anachosema kuwainspire mashabiki wake.

“Thanks God for my new GOLD & DIAMONDS collection…i never thought i would be able to hang 50,000$ on my neck,” ameandika kwenye picha ya kwanza.

Kwenye picha nyingine ameandika, “Thanks God for your daily blessings never thought i would be able to walk with 22,000 $ on my Hand!!!… jus get inspired @sallam_sk don’t hate.”

Muimbaji huyo wikiendi iliyopita alitumbuiza show ya nguvu humo Muscat, Oman.
Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top