Polisi wafanikiwa kumkamata Dkta Mwaka, bofya hapa kujua zaidi

Jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni tabibu Juma Mwaka, maarufu Kama Dokta Mwaka, baada ya kumsaka Kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Polisi yasema mmiliki wa Foreplan Clinic tabibu Juma Mwaka amejisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi Dar leo, atakiwa kurudi kesho kwa mahojiano.

Jeshi la polisi linatekeleza agizo la Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuwa tabibu huyo mashuhuri akamatwe Kwa kukiuka agizo la Serikali la kuacha kutoa huduma za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa kibali na Baraza la tiba asili na tiba mbadala, ambao walimkuta na hatia ya kukiuka masharti ya sheria ya tiba asili na tiba mbadala ya Mwaka 2002,

sheria namba 23, ulaghai wa kujiita dokta na kujifanya amesomea tiba ya kisasa kumbe la, kukutwa na shehena ya dawa za kisasa zaidi ya boksi 200 bila vibali vya mamlaka ya chakula na dawa, TFDA na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala kinyume cha sheria, haswa baada ya kufutiwa usajili wa kutoa huduma hizo. Tabibu Mwaka alikuwa Polisi Kwa mahojiano katika kituo cha kati.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top