Akifungua mkutano huo Katibu mkuu wa CHADEMA Vincent Mashinji amezungumzia umuhimu wa operesheni yao walioiita UKUTA, amedai kuna Ombwe kubwa la uongozi katika taifa kutokana na yanayoendelea sasa hivi
Amesema kuna barua amabazo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Mwanasheria wa chama Tundu Lissu ambazo wamezipata wakitakiwa wajieleze kwenye tume ya maadili ya viongozi.
Barua hiyo inadai kiongozi wa upnzani bungeni amekiuka hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.
Barua hiyo inaendelea kusema mwezi Julai mwaka 2016 Mbowe alitoa matamshi ambayo yanachochea wananchi kutokutii sheria za nchi na kudharau misingi ya kidemokrasia iliyopo nchini ambayo yalikuwa hayazingatii misingi ya demokrasia na kukiuka hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma aliyosaini 29/12/2015 na kukubali kuyatekeleza.
Mbowe ametakiwa kutoa maelezo ni kwanini asichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka kama kiapo cha ahadi kinavyotanabaisha ndani ya siku 21 toka tarehe ya kupokea barua hiyo, kushindwa kufanya hivyo itapelekea kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yake Barua hiyo imesainiwa na Jaji mstaafu Salome Esther Kaganda kamishna wa maadili.
Katibu mkuu akizungumzia barua hiyo amesema CHADEMA sio kikundi cha watu wachache bali ni chama cha siasa kilichosajiliwa kinachotakiwa kuwa na wanachama mia mbili kila mkoa, akiendelea kusema kina wabunge karibia theluthi moja na kupata asilimia 40 ya kura na madiwani 1189 na kuongoza halmashauri za majiji yote kasoro jiji la Mwanza.
Amedai lugha iliyotumika kwenye barua aliyooandikiwa Mbowe si ya kuandikiwa kiongozi wa chama Kikubwa cha siasa ambaye pia amechaguliwa na wananchi wa jimbo lake kwa kura nyingi.
Post a Comment