Kiwanda cha sukari cha TPC Kilimanjaro cha anza kuzalisha sukari


Kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo mkoani Kilimanjaro kimeanza uzalishaji wa sukari leo ambapo msimu huu wanatarajia kuzalisha tani laki moja na sita ambazo zitagawanywa kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya Kaskazini na hatimaye kuondoa kabisa tatizo la ukosefu wa sukari sokoni.

Afisa mtendaji mkuu na utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC Bw.Jafary Ally amesema baada ya kumaliza ukarabati na uwekezaji wa kiwanda hicho ambao uligharimu kiasi cha dola laki tano na nusu,kwa sasa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 450 za sukari kila siku sawa na ongezeko la asilimia 10.

Amesema uzalishaji huo ni mkubwa na kwamba sukari hiyo itaanza kusambazwa June 18 mwaka huu kwa bei elekezi ambapo mkoa wa Kilimanjaro utapatiwa tani 100, Arusha tani 100 na Manayara tani 70 na sukari itakayobaki itasambazwa katika mikoa ya Tanga na Singida.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw.Said Meck Sadick  amesema kwa wasambazaji na wauzaji wa rejereja ambao watakiuka agizo la kuuza sukari kwa bei elekezi ya serikali watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Baadhi ya wafanyabishara wa sukari mkoani Kilimanjaro wameuomba uongozi wa kiwanda cha sukari TPC kuangalia uwezekano wa kuruhusu wafanyabiashara kuchukua sukari kiwandani badala ya mawakala pekee hali ambayo wanasema  itasaidia kuondoa tatizo la sukari kupandishwa bei hiholela.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top