Jeshi la Polisi limejipanga kupambana na aina mpya ya uhalifu wa makundi ya watu yenye silaha za moto uliongia nchini ambao uvamia maeneo mbalimbali yakiwemo ya biashara na kufanya uhalifu wa uporaji fedha,silaha na kusababisha mauaji ya askari na raia wema.
Kauli hiyo jeshi la polisi imekuja ikiwa ni sikuchache baada ya kundi la watu wenye silaha kuvamia ACCESS BENKI tawi la Mbagala rangi tatu na kupora fedha na kusababisha vifo vya watu saba wakiwemo Polisi.
Akizungumzia mipango ya jeshi hilo,mkuu wa operesheni na mafunzo wa jeshi la Polisi kamishna Sato Marijani amesema nchi nyingi zinashirikiana kukabiliana ya makundi uhalifu ambapo hapa nchini baadhi ya vijana walishakamatwa wakiwa njiani kwenda kupata mafunzo ya kujiunga na makundi hayo.
Aidha kuhusu matumizi ya bodaboda katika kutekeleza uhalifu, kamishna marijani amewataka madereva bodaboda kutoa ushirikiano katika operesheni maalum dhidi ya watu wanaochafua biashara ya bodaboda kwa kuzitumia kutekeleza uhalifu na kusisitiza jeshi la polisi linatahakikisha linawakamata watu wote wanafanya uhalifu kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.
Post a Comment