Tamisemi yawataka watendaji mkoani Arusha kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu waziri wa Tamisemi Bw.Suleimani Jaffo amemtaka katibu tawala wa mkoa wa Arusha kumpatia orodha ya watendaji wanaoendelea kufanya kazi kwa mazoea na kusababisha wananchi kuteseka bila sababu za msingi ili hatua zikiwemo za kuwafukuza kazi zichukuliwe haraka kwani wakati wa kubembelezana umekwisha.
Mh.Jaffo ameyasema hayo baada ya kupewa taarifa inayopingana na hali halisi ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali likiwemo la kushughulikia maafa yanayowapata wananchi iliyosababisha baadhi ya watendaji kushindwa kujieleza na wengine kutupiana lawama na kuikana maelezo yao wenyewe.
Mkanganyiko wa watendaji hao ulikuja baada ya naibu waziri Mh.Jaffo kutaka kupata maelezo ya watendaji hao wanavyoshughulikia majanga mbalimbali yanayowapata wananchi likiwemo la kuezuliwa kwa shule ya msingi isimani lililotokea Desemba mwaka jana ambalo hadi sasa hatua hazijachukuliwa licha ya kuwa ndani ya uwezo.
Katika sakata hilo kadiri viongozi na watendaji hao walivyojaribu kutoa maelezo yaliendelea kutofautiana jambo ambalo Mh.Waziri.Jaffo amesema linalodhihirisha wazi kuwa lipo tatizo ambalo serikali haiwezi kuendelea kulifumbiwa macho.
Mh.Naibu waziri Suleiman Jaffo alifanya ziara ya kushtukiza mkoani Arusha ambayo inadaiwa kuwa ni matokeo ya malalamiko ya wannachi wakiwemo wanaopatwa na maafa ama majanga mbali mbali ya kuchelewa kupata msaada wa serikali licha ya kupewa ahadi kila janga linapotokea.
Post a Comment