MSHIKEMSHIKE YA UCHAGUZI ZANZIBAR

Tume ya uchaguzi ZEC yasema wagombea wote ni halali na watagombea nafasi zao.

Wakati baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza kujitoa uchaguzi wa marudio Zanzibar, tume ya uchaguzi -ZEC- imetoa msimamao wake na kusema wagombea wote ni halali na watagombea nafasi zao kwa vile hakuna hata chama kimoja kilichofuata sheria na kanuni za uchaguzi.

Msimaamo huo wa tume umetolewa na mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo amesema kuna utaratibu wakujitoa na kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi hakuna chama kilichofuata kanuni ikiwa ni pamoja na wadhamini wawagombea kutangaza kuondoa udhamini wao, hivyo wagombea wote wa urais, uwakilshi na udiwani wote bado ni halali.

Akizungumzia maandalizi hayo amesema yanaenda vizuri ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi, upangaji wa vifaa, mawasilaino na vyama na uchapishaji wa dafatri na mafunzo na wagombea kuanza kupatiwa ulinzi na haki zote kwa mujibu washeria huku akielzea karatasi za kura amabzo zinachapwa nje zinatarajiwa kuwasili mapema mwezi ujao.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi vyama amabvyo vimethibitisha kushiriki ni pamoja na CCM, TADEA, ADC, CCK, AFP, SAU, TLP, huku CUF, NRA, CHAUMA, DP, Jahazi asilia na ACT Wazalendo ambao mgombea wake Khamis Lilla ametangaza kugombea huku chama chake kikimufukuza uanachama.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top