Mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amewaagiza madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wanaotokana na vyama vinavyounda umoja wa katiba (UKAWA) ambao unaongoza manispaa hiyo kuhakikisha wanawashirikisha wananchi katika kila hatua inayofikiwa inayohusiana na mchakato mzima wa mradi wa ujenzi wa soko kuu jipya la Bukoba.
Ametoa agizo hilo baada ya kutembelea soko la sasa la mji wa Bukoba ambalo ujenzi wake ulikwama kutokana na migogoro iliyojitokeza miongoni mwa madiwani wa manispaa hiyo ambao ulipekelekea baadhi ya madiwani kugomea vikao kwa zaidi ya miaka miwili jambo lililopelekea baadhi yao kuvuliwa nyazifa zao za udiwani kwa amri ya mahakama, Mbowe amesema kuwashirikisha wananchi katika utekelezwaji wa miradi wa soko kuu la Bukoba ni namna ya kuweka mambo wazi jambo linalopunguza migogoro isiyo na tija ndani ya jamii.
Post a Comment