Maisha tunayoishi ni kama tuna wake wanne.
1. Mke wa nne ni mwili wako, tunatumia gharama kubwa kuupendezesha na kuutunza uonekane wa kuvutia lakini hatuendi nao popote wakati wa kufa, unayarudia mavumbi yake.
2. Mke wa tatu ni malizetu, hadhi na utajiri. Japo tunahangaika kuvitafuta, tunapokufa hatuendi navyo popote..wanabaki navyo wengine.
3. Mke wa pili ni familia zetu na marafiki. Hata wakitupenda na kuwa karibu nasi kiasi gani, hawawezi kufa na sisi, watakachoweza kufanya ni kutusindikiza hadi makaburini na sio zaidi ya hapo!!!
4. Mke wa kwanza ni Maisha yetu ya kiroho. Yenye manufaa makubwa ya uzima wa milele, ambao katika harakati zetu za maisha na azma yetu ya kutafuta utajiri wa mali na raha za dunia tumeutupa mbali.
Mungu akusaidie kujali na kushibisha Roho yako zaidi ya vingine vyoote.
Mshirikishe na mwenzio.
Post a Comment