Kama bado ujaelewa makato ya asilimia 18 yanakatwa vip, ebu bofya hapa

Hii ni taarifa kutoka Tanzania Revenue Authority (TRA) na gazeti la The Citizen wakieleza jinsi makato ya asilimia 18% yatakavyokuwa yakikatwa, wamesema hivi!

Ukweli nikuwa kiasi cha tozo la ongezeko la thamani yaani VAT kitakachotozwa ni asilimia 18 ya kiasi cha gharama za huduma iliyotolewa na benk au tasisi yeyote ya fedha.

Kwa mfano, Ada ya huduma ya benk ambayo ametozwa mteja ni Tsh 1,000/= kodi ya ongezeko la thamani itakayotozwa kwenye kiasi hiki ni Tsh 152.50 tu na benk husika itabaki na kiasi cha Tsh 847.50

Kiwango hiki cha shilingi 152.50 ndicho kitakachorejeshwa serikalini na benk au tasisi ya fedha baada ya kupunguza kodi ya ongezeko la thamani iliyolipwa kwenye manunuzi ambayo yamefanywa na benki au tasisi ya fedha husika.

Kwa mujibu wa sheria hii, kodi ya ongezeko la thamani VAT haitatozwa kwenye riba inayotozwa na benk kwenye mikopo.

Aidha kuna maelekezo yametolewa na moja ya benk hapa nchini kuwa mtumiaji wa huduma za ifedha atatakiwa kulipia kwa fedha taslimu kama muamala husika haukupitia kwenye akaunt.

Taarifa hii si sahihi kwa kuwa ukusanyaji wa VAT husika utafanywa kwa njia ile ile ambayo gharama za huduma za kifedha zinakusanywa kama ilivyo kwa sasa.

Mamlaka ya mapato tanzania itatoa maelekezo yanamna ya utoaji wa risiti za kielectronic utakavyofanyika ili kuiwezesha benk au tasisi ya kifedha kutimiza matakwa ya kisheria ya kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 2014 kama ilivyo lekebishwa kwa mwaka 2016.

Hivyo kupitia taarifa hii tunazitaka benk na tasisi za fedha zilizoamua kwa makusudi kutoa taarifa zisizo sahihi kwa umma kuacha mara moja vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Kimsingi benk na tasisi za fedha zinazohusika zinaagizwa kurekebisha mara moja taarifa walizokwisha zisambaza ili zibebe maudhui sahihi ya marekebisho ya sheria hii.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Desgned By MTM Mikoa Yetu Published.. Blogger Templates
Back To Top