CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO <CHADEMA>
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU ILIYOFANYIKA HOTELI YA BAHARI BEACH LEDGER PLAZA ,23-26 JULAI, 2016.
1.0 UTANGULIZI
Kamati Kuu ya dharura ya Chama iliketi kuanzia 23-26 Julai ,2016 Jijini Dar es salaam na ilikuwa na ajenda moja mahsusi ambayo ni kujadili hali ya siasa na uchumi wa Taifa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani mwenzi Novemba ,2015.
Mwenendo wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano ,chini ya Raisi John Magufuli ,ni dhahiri kuwa umeamua kuiweka demokrasia kizuizini na kuleta utawala wa Kidektteta katika nchi yetu.
2.0 MATUKIO MAHSUSI YA UKANDAMIZAJI WA HAKI NA DEMOKRASIA NCHINI
2.1-Kupiga marufuku mikutano ya Vyama vya siasa.
Serikali kupitia Waziri Mkuu hatimaye Raisi na jeshi la Polisi walitangaza kwa nyakati tofauti kwamba ni marufuku kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa mpaka mwaka 2020 ili kuipa serikali nafasi ya kufanya kazi.Huu uvunjaji wa Ibara ya 20 <1>ya Katiba.
Aidha katazo hilo la mikutano ya siasa linakiuka Sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 11 ambayo imetoa haki kwa vyama vya siasa kufanya kazi ya siasa.
2.2 Kupiga Marufuku urushaji wa moja kwa moja <live coverage>wa mijadala ya bunge .Katazo hilo ni kinyume na Katiba ibara ya 18 ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambayo inatoa uhuru wa maoni na uhuru wa kupata habari kwa kila mwananchi .
2.3 Kudhibiti Wabunge wa Upinzani bungeni -Serekali imejificha nyuma ya kiti cha Naibu Spika wa bunge ,Dkt.Tulia Ackson Mwansasu <Mb> ili kuwathibiti wa upinzani Bungeni kwa lengo la kuwanyamazisha wasiikosoe serikali.
Ikumbuke kwamba Dkt.Tulia akiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa mtumishi wa umma asiyepaswa kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa;lakini ghafla anaonekana akigombea nafasi ya Naibu Spika kupitia CCM.Hivyo yupo Naibu Spika ambaye ni mteule wa Rais.Swali Anawajibika kwa nani kati ya Bunge na Raisi?
2.4 Kuingilia Mhimili wa mahakama -Serikali ya CCM kupitia Raisi ;kwa nyakati tofauti imeonekana kujaribu kuingilia uhuru wa Mahakama jambo ambalo ni hatari kwa utoaji wa haki nchini.Katika hotuba yake,wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria duniani Raisi alinukuliwa akisema kwamba Mahakama iwahukumu harakaharaka watu waliokwepa kodi halafu atatumia asilimia Fulani ya fedha ambazo zitakuwa zimepatikana kutokana na wale walioshindwa kuwapa mahakama .
2.5 Kupuuza Utawala wa Sheria -Tarehe 24 Juni ,2016 wakati wa uzinduzi wa siku ya usalama wa raia,Raisi Magufuli alinukuliwa akiwaruhusu polisi kuwaua majambazi bila kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.Aidha aliuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kuwapandisha vyeo wakataowauwa majambazi.
2.6 Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari-Serikali imepeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Haki kupata habari.
Sheria hii imeweka adhabu kubwa sana kwa waandishi kama vile kifungo cha miaka 15 na kisichozidi miaka 20 kwa mujibu wa kifungu cha 6<6>
2.7 Serikali hii inatishia ukuaji wa uchumi
Tangu serikali ilipoingia madarakani hali ya ukuaji wa uchumi na uwekezaji wa mitaji imekuwa ikiporomoka kwa kasi kubwa sana nchini mwetu na hata baadhi ya wawekazaji wanaondoa mitaji yao kutokana na serikali hii kukosa mwelekeo unaoeleweka wa kiuchumi.
2.8 Serikali za mitaa kunyanganywa mapato na serikali kuu.
Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 tulifanikiwa kushinda maeneo ya Majiji ya DSM,Mbeya ,Arusha na Miji mikubwa ya Iringa,Moshi ,Bukoba ,Babati Tunduma na mengineyo ya maeneo ya mijini ambayo kwa kiasi kikubwa wanategemea sana kuendesha Halimashauri hizo kwa kutumia kodi ya Majengo inachangia kati 30% hadi 60% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Miji.
Post a Comment