Fuata maelekezoyaliyopo hapo juu ili kuweza kushiriki promotion ya kushinda simu.
Wakazi wa kijiji cha Likonde kata ya Mayanga mkoani Mtwara, wameiomba serikali kuwatatulia kero kubwa ya maji inayowalazimu kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 5 kupata maji, ambayo hata hivyo, sio salama kwa afya zao.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kijiji hicho, baadhi ya wakazi hao wamesema wamekuwa wakitegemea kupata maji toka mradi mkubwa wa maji wa mbuo, unaohudumia vijiji 11 katika kata 4 za Mayanga.
Muungano, Naumbu na Mkunwa, lakini mradi huo imeshindwa kuwaletea maji, na hivyo wakazi hao kulazimika, ama kutembea kilometa 5 kutafuta maji au kununua toka kwa wafanyabiashara wanaoleta maji kwa malori kijijini hapo ndumi moja shillingi 500, hali inayowaongezea umaskini, na hivyo kumwomba waziri wa maji kutembelea mradi huo ili kutafuta ufumbuzi.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa kijiji hicho cha Likonde Said Mohamed amekiri kijiji kukabiliwa na tatizo kubwa la maji, na kuiomba serikali kuuchukua mradi huo wa maji wa Mbuo na kuuendesha, kwa kuwa bodi ya wadhamini inayosimamia mradi huo imeshindwa na kusababisha ukosefu mkubwa wa maji. Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa mradi huo wa maji wa Mbuo hakuweza kupatikana.
Fuata maelekezo yaliyopo hapo chini ili kuweza kushinda simu ya mkononi.
Post a Comment