Kwanza nianze kwa kuishukuru sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutujengea vituo bora vya kushusha na kupakia abiria kikiwemo kituo cha kariakoo.
Lakini mbali na hayo ya serikali kutufanyia mambo mazuri limejitokeza tatizo ambalo linatupa shida sana sisi kama wakazi wa maeneo ya Mbagala.
Tangu kituo kipya cha kariakoo kufunguliwa kumejitokeza tabia ya madreva na makondakta wanaotoa huduma ya usafirishaji kwa wakazi wa Mbagala kuingiza magari yao kituoni kisha wanawakataza abiria kupanda magari hayo, wakiulizwa wanasema hawapakii, na tabia hii waga inatumiwa nyakati za jioni kuanzia mda wa saa 5:00
Tabia hii inafanywa na baadhi ya madreva kwa kushirikiana na makondakta wao lengo lao nikukataa kuwapakia abilia wachache ndio maana wanasema hawapakii, watu wanarundikana kituoni mpaka watakapokuwa wengi ndipo wanawapatia.
Tabia hii sio nzuri maana kila abilia anakuwa na majukumu yake sasa unapomkatalia asipande gari lako unategemea nini kitatokea?
Sisi kama abiria tunasema kufanya hivi ni kutunyanyasa sisi watumiaji wa magari yao, kwaiyo tunaomba police wa pale kamata waweze kutusaidi juu ya tabia hii.
Post a Comment