Waziri mkuu Kassim Majaliwa : Rais hakukosea kuzuia sukari kuingia nchini kiholela
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kauli ya Rais John Pombe magufuli ya kuzuia kuingizwa kwa sukari kiholela nchini ilikuwa ni katika kulinda viwanda vya ndani.
Aidha Majaliwa amesema kuingia kwa sukari Tani 70,000 toka nje ya nchi hakutaathiri uzalishaji wa viwanda unaotarajiwa kuanza mapema mwezi julai.
Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe, Majaliwa amesema uhaba wa sukari ni tani 100,000 na uwezo wa viwanda kuzalisha ni tani 320,000 huku mahitaji ya sukari kwa mwaka mzima ni tani 420,000.
Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini, Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.
Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi. Mhe. Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada lilipo katika mto Rufiji.
Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.
Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.
Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika. Kuhusu bei elekezi ya sukari, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.
Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika.
Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kuto ka zinapoagizwa na kumfikia mlaji.
Post a Comment